Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe Dk.Ali Mohamed Shein Ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiongoza   Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na (kulia) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.

Na.Is-haka Omar - Zanzibar.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais mstaafu wa Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein leo ameongoza kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho cha siku moja kimeanza saa 4:00 asubuhi katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui ambapo kimehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa mbalimbali za kiutendaji kutoka katika idara za CCM Zanzibar.

Mbali na hilo,kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Hussein Ali Mwinyi aliyoifanya katika mikoa sita ya CCM Kichama.

Katika kikao hicho cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar kimetoa azimio la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa maamuzi yake ya kuwarejeshea fedha zao wananchi waliokuwa wanaidai kampuni ya Masterlife.

Mbali na hilo kikao hicho cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar imempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani, na kuridhishwa na uongozi wake wenye mafanikio makubwa yakiwemo kudumisha hali ya amani,utulivu na mshikamano kwa wananchi wote.

Kikao hicho ni cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977 Toleo jipya la mwaka 2017,Ibara ya 108 (2),inayofafanua kwamba Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja kila miezi mitatu.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.