Habari za Punde

Timu ya mkoa wa Magharibi na mkoa wa Pwani zimefanikiwa kutinga fainali ya mashindano ya Green cup yaliyoandaliwa na UVCCM.

Katika mtanange wa nusu fainali iliyowakutanisha Timu ya Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Tabora, ambapo mkoa wa pwani umeitandika mkoa wa tabora kwa bao 4 za mikwaju ya Penalti dhidi ya Timu ya tabora iliyopata bao 3, baada ya kutoka uwanjani katika dakika 90 bila ya kufungana.

Katika michuano hiyo ya nusu fainali ya pili iliwakutanisha timu ya Mkoa wa Magharibi na mkoa wa morogoro, ambapo timu ya mkoa wa Magharibi iliichapa bao mbili timu ya mkoa wa morogoro, bao la kwanza likiwekwa wavuni na mchezaji Ibrahim Hamad hilika mwenye jezi  nambari saba katika dakika ya 16, na bao la Pili kuwekwa wavuni na Mudathiri Diara mwenye jezi nambari 14 mgongoni.

Akitoa salamu zake katika michuano hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarijika kuona nusu fainali hiyo inachezwa Zanzibar jambo ambali linatoa fursa kuitangaza Zanzibar kimichezo.

Mhe. Hemed ambae pia ni mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM ameupongeza umoja wa vijana kwa kuanzisha michuano hiyo, ambayo inaonesha wazi kuunga mkono utekezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 kukuzaji michezo nchin Tanzania.

Kwa upande wake katibu mkuu wa UVCCM Taifa kenan Kihongosi amesema lengo la kuanzisha michuano hiyo ni kuwaunganisha vijana wote wa Tanzania kuwa na uhusiano mzuri kupitia michuano hiyo.

Fainali ya mchezo wa Green Cup inatarajiwa kuchezwa Disemba 12 mwaka huu katika Dimba la Mkapa Jijini Dar-es-salaam  ambapo Timu ya Mkoa wa Pwani itakutana na Timu ya Mkoa wa Magharibi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.