Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla akikabidhi Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira katika kikao kilichofanyika leo tarehe 10/12/2021 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Bw.
Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na
Usafi wa Mazingira akionyesha Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na
Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla leo tarehe 10/12/2021, jijini Dar es Salaam.
Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira akiendesha kikao mara baada ya kupokea Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira leo tarehe 10/12/2021, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya
Hifadhi na Usafi wa Mazingira kutoka katika taasisi mbalimbali
ikiwa ni pamoja na Sekta Binafsi, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Mashirika ya
Kimataifa, Asasi Zisizo za Kiserikali, na Taasisi za Fedha. Kushoto ni Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya
Kampeni Kabambe na Bw. Faraja Ngerageza Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo leo tarehe 10 Disemba, 2021 amekabidhi Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake
iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis
Abdulla, amesema Lengo la Kampeni hiyo ni kuelimisha na kuhamasisha ushiriki wa
jamii na uwajibikaji wa mamlaka za usimamizi katika hifadhi na usafi wa mazingira ili
kuleta ustawi wa jamii ya watanzania na maendeleo endelevu.
Katika kufanikisha
utekelezaji wa Kampeni hiyo, Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Mpango Kazi wa
Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira wa Kipindi cha Miaka Mitano
2021-2026, Mwongozo wa Tuzo ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na Rasimu ya
Mkakati wa Kutafuta Fedha za kuwezesha utekelezaji wa Kampeni Kabambe ya
Hifadhi na Usafi wa Mazingira.
“Nyaraka hizi ni vitendea
kazi vya Kamati hii Maalumu pamoja na jamii ya watanzania katika utekelezaji wa
Kampeni hii. Hivyo ninawakabidhi rasmi nyaraka hizi muhimu kama ishara ya kuwa
kazi imeanza rasmi. Niwaombe mtoe
uzito wa pekee katika kutekeleza majukumu hayo ya hiari ili kuwezesha kufikiwa
kwa lengo la Kampeni” Jafo alisisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe Bw. Seif Ally Seif amesema kwamba, ni
imani yake kuwa utekelezaji wa Kampeni hiyo utaanza mara moja na kuwa Kamati
yake iko tayari kuungana na Serikali katika kuwezesha utekelezaji wake kwa
ufanisi mkubwa.
Kampeni Kabambe
ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira ilizinduliwa tarehe 5 Juni, 2021 wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya
Mazingira Duniani na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Kampeni hii itakuwa endelevu na itatekelezwa
katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021 hadi 2026.
Wajumbe hawa wa Kamati Maalumu
wanatoka katika taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sekta Binafsi, Serikali
Kuu, Mashirika ya Umma, Mashirika ya Kimataifa, Asasi Zisizo za Kiserikali, na
Taasisi za Fedha.
No comments:
Post a Comment