Habari za Punde

Kikosi kazi cha kutokomeza kipindupindu Zanzibar chatakiwa kuwasilisha taarifa zenye uhalisia

 Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar. 07/01/2022.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni  ya Kukabiliana na Maafa Makame Khatib Makame amewataka Wajumbe wa kikosi kazi cha kutokomeza kipindupindu Zanzibar,(ZACCEP) kuwasilisha  taarifa zenye uhalisia wa utendaji wa kazi zao.


Akiyasema hayo katika Ukumbi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Maruhubi, wakati wa kikao cha siku moja kinachohusu utoaji wa taarifa za utekelezaji wa mpango kazi wa kipindi cha Julai hadi Septemba 2021, kwa wajumbe wa Mpango huo.


Alisema utoa wa taarifa hizo kwa wajumbe ambao wanaziwakilisha Taasisi zao zinatakiwa ziwe sahihi jambo ambalo litarahisisha ufuatiliaji  wa utekelezaji huo


Aidha alisema mashirikiano ya pamoja yanahitajika kwa Taasisi zilizomo katika mpango huo ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya kuhakikisha lengo la miaka kumi ya kutokomeza kipindupindu linafanikiwa Zanzibar.


 “Tukifanya kazi kwa pamoja na kila mmoja kuona kwamba tuna jukumu la msingi, kuhakikisha usafi, afya na mazingira vinatekelezwa ipasavyo sambamba na kupatikana kwa huduma za msingi katika jamii kutasaidia kukabiliana na maradhi haya, “alisema Mkurugenzi.


Nao Muakilishi Mkaazi  wa  Shirika la Afya ulimwenguni  (WHO)  aliopo Zanzibar Dr. Emma Bisamaki pamoja na Muakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto  (UNICEF) aliopo Zanzibar Mr Marko Msambazi walisema wameridhishwa na hatua mbali mbali za  utekelezaji wa mpango huo ambao utahakikisha ifikapo 2027 maradhi ya kipindupindu iwe historia kwa Zanzibar .


 Walisema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua mbali mbali za  hutoa huduma kwa jamii  ili kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata afya bora.

 

Kwa upande wa Wajumbe hao walisema katika kuhakikisha wanaweka mazingira ya mji safi wameazisha  vikundi vya uzoaji taka katika kila shehia kwa lengo la kudhibiti taka na kuweka haiba nzuri katika mitaa.


walifahamisha kuwa wanaendelea kutoa elimu mbali mbali kwa jamii jinsi ya kuzisarifu taka kuwa malighafi kwa kufanya makaa,,mbolea na karatasi jambo ambalo litawasaidia vijana wengi kupata ajira.


Walieleza katika kazi zao hizo pia kuna changamoto mbali mbali  zinazojitokeza ikiwemo ukuwaji wa miji mipya katika maeneo mbali mbali hili  linachangia uzalishaji mkubwa wa taka jambo ambalo  hupelekea uhaba wa vitendea kazi ikiwemo gari za kubebea taka hizo .

 Vile vile jamii kuchimba visima bila ya utaratibu wa mamlaka husika hali hii husababisha kutumia maji yasiyo salama kutokana na ukaribu wa makaro ya vyoo ,


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.