Habari za Punde

MANGULA AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Ndugu Philip Mangula, akipokea salaamu maalum za pongezi za miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM kutoka kwa Chama Cha Kikomunisti cha Cuba, zilizowasilishwa na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hernandez (kushoto), leo 24/2/2022, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam. Pia, Balozi Hernandez alimuaga Ndugu Mangula kufuatia kumalizika kwa muda wake wa kuiwakilisha Cuba nchini Tanzania
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Ndugu Philip Mangula, akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hernandez (kushoto), ambaye alifika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, kwa lengo la kumkabidhi salamu za pongezi za CCM kutimiza miaka 45, kutoka Chama Cha Kikomunisti cha Cuba na kuagana naye baada ya kumaliza muda wake wa kuiwakilisha Cuba nchini Tanzania. (Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.