Habari za Punde

WAZIRI NDUMBARO AMPONGEZA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI, ATAKA KUKUA KWA DIPLOMASIA YA UCHUMI KATIKA UTALII

Na.Mwandishi Maalum. New York Marekani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuweka nguvu za kutosha  katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ikiwemo kuwavutia watalii kutoka nje ya nchi kuja nchini.

Ametoa kauli hiyo leo wakati mara baada ya kufanya ziara ya  kutembelea ofisi ya Ubalozi huo ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na Watumishi na Wawekezaji mara baada ya kumalizika kufanyika kwa mkutano wa 50 wa mwaka wa uwindaji wa kitalii uliofanyika katika Jiji la Las Vegas nchini Mareakani.

Akizungumza na timu ya Watumishi hao, Dkt. Ndumbaro amempongeza Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza kwa kazi kubwa anayoifanya ya Diplomasia katika tasnia ya biashara na utalii.

" Nimevutiwa mno kwa jinsi unavyoitendea haki Diplomasia ya uchumi natamani Mabalozi wwngine wanaioziwakilisha nchi zetu nchi za nje wajifunze kutoka kwako" amesisitiza Dkt.Ndumbaro

Ambapo amewataka Wanadiplomasia hao kuwa daraja katika  kuwawezesha watalii kuja  nchini Tanzania 

Dkt.Ndumbaro amesema Diplomasia ya uchumi katika tasnia ya utalii inapaswa  kutangaza na kujibu maswali ya watu mbalimbali wanaotaka kutalii Tanzania kuhusu namna ya kufika nchini kiujumla na katika kila kivutio cha utalii kimahususi.

"Kutokana na kasi kubwa ya maendeleo ya kiuchumi, Mabalozi  wanaoziwakilisha nchi Diplomasia ya kiuchumi ndo injini ya maendeleo haikwepi, ongezeni ujuzi katika eneo hili." amesisitiza Dkt. Ndumbaro.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi hao kuwa mstari wa mbele katika kujua masuala ya uwekezaji na biashara pamoja na mambo yote muhimu kuhusu utalii nchini ili waweze kuwaelezea wananchi wanaowahudumia

Vilevile amewataka Wanadiplomasia hao kuwa kichocheo cha  watalii kutoka katika nchi waliyopo kuhudhuria katika mikutano, makongamano na maonyesho ya utalii ya ndani ya Tanzania ikiwemo 
matamasha ya kiutamaduni .

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amemwalika nchini Tanzania, Kiongozi wa Vyama vya Waongoza Watalii nchini Marekani, Rumit Mehta kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko Ukanda wa Kusini 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.