Habari za Punde

ZMA Yafanikiwa Kusajili Meli za Kigeni 44 Ndani ya Kipindi cha Miezi Minne.

Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini imefanikiwa kuwa na ongezeko zaidi la usajili  wa meli na kupelekea kuingizia Serikali mapato.

Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Ndugu Sheikha Ahmed Mohamed ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari afisini kwake Malindi Jijini  Zanzibar.

Mkurugenzi Sheikha amesema katika kipindi cha mwezi Novemba hadi Januari jumla ya meli Arobaini na nne (44) zimesajiliwa  na kuiingizia Selikali Mapato ya Shilingi Milioni Miatatu kumi na Tisa, Mia Tano na Kumi Sita (319,516,000.00) ambapo hadi sasa fedha  zilizokwisha kukusanywa  zinafikia Shilingi Milioni  mia Moja Kumi Nane laki Saba Ishirini na Sita (118,726000.00).

Akifafanua kuhusiana na usajili huo amesema mwezi wa November wamesajili meli 14,December Meli 14,Januari Meli 12 na Februari meli 4 ikiwa na jumla ya meli 44 ambapo alisema Mamlaka inafanya juhudi za makusudi kushajihisha nchi nyenyngine Duniani kuja kusajili Meli zao Zanzibar kwa lengo la kuiengezea mapato Serikali.

Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyu amesema Mamlaka ya Usafiri Baharini imefanikiwa kudhibiti kupanda kwa bei ya   nauli mara kwa mara kwa abiria wanaosafiri kutoka  Unguja kwenda Dar es salaam na wanaosafiri kutoka Uguja kwena Pemba. 

Hata hivyo amefafanua kwamba  mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wadau imepiga hatua katika udhibiti wa Usalama wa vyombo vya baharini jambo ambalo lililopelekea kuepusha kutokea kwa ajali za meli ambapo meli zote zinapakia abiria kwa mujibu wa idadi inayohitajika.

Akizungumza kuhusiana na suala la Mabaharia Mkurugenzi huyo amesema mamlaka imeruhusu kampuni ya Danausi kuajiri mabaharia wa Kizanzibar na Tanzania kwa ujumla jambo ambalo kwa namna moja au nyengine imepelekea benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) kuingiza fedha za kigeni kutokana na mishahara inayoingizwa katika Akaunti za mabaharia hao.

Katika mikakati ya baadae Mkurugenzi ameseama mamlaka ina mpango wa  kuongeza usajili wa vyombo vya Usafiri  baharini na mizigo vyenye uwezo wa mwendo kasi kama ilivyo kwa safari za Unguja na   Dar –es –salaam sambamba na kuongeza safari kutoka Pemba kwenda Tanga.   
 
Imetolewa na Kitengo cha Habari (WUMU)
Febuari 15, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.