Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Mabunge ya Afrika, Mussa Kombo Bakar amesema dhana mpya ya ufuatiliaji wa sheria inatarajiwa kufanyiwa kazi ili kuhakikisha sheria zinazopitishwa zinatekelezwa ipasavyo.
Amesema suala la kufuatilia sheria ni moja ya jambo la msingi la kuhakikisha sheria zinaz otungwa zinatekelezwa .
Hayo ameyasema katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi Chukwani wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kikao cha siku mbili cha Kamati Tendaji ya chama cha Wanasheria wa Mabunge ya Afrika ambacho kinatarajiwa kufanyika leo hapa Zanzibar.
Aidha alisema kumekuwa na udhaifu wa utekelezaji wa sheria kwamba sheria nyingi zinazotungwa hazifanyiwi kazi .
Alifahamisha kuwa lengo la Mkutano wa kamati hiyo ni kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanasheria wote wa Mabunge ya Afrika ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu .
Alifahamisha kuwa azma ya kuundwa chama hichi ni kubadilishana uzoefu pamoja na kuongeza ujuzi miongoni mwa Wanasheria wa Mabunge mbali mbali ya afrika
Chama cha Wanasheria wa Mabunge ya Afrika kimeanzIishwa mwaka 2011 nchini Nairobi Kenya ambacho kimekusanya Wanasheria wa Mabunge mbali mbali wa afrika.
No comments:
Post a Comment