Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Azungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, leo Machi 7, amekutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) Bi.Salma Ali Hassan. 

Bi.Salma amefika ofisini kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Migombani Mjini Zanzibar, kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, kushika nafasi hio hivi karibuni.

Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
07/03/2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.