Habari za Punde

SMZ yajizatiti kupunguza bei za mafuta

 


Na Mwashungi Tahir         Maelezo      

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inaendelea  na kufanya jitihada zake   kupunguza makali ya bei za mafuta kwa wananchi wake ili waweze kuzimudu bei hizo.

Hivyo Serikali imeendelea kupunguza makali ya bei kwa kufidia jumla ya TZS 298 kwa lita ya mafuta.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  huko katika ukumbi wa Maisara juu ya mabadiliko  ya bei za mafuta kaimu M kuu wa Kitengo cha uhusiano Hassan Juma Amour  kutoka Mamlaka ya Udhibiti na Huduma za Maji na Nishati ZURA  amesema bei za mafuta zimeendelea kuongezeka katika soko la Dunia.

Amesema bei hizo zinatokana na wastani wa mwenendo  wa mabadiliko wabei za mafuta katika mwezi wa February 2022 kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa March 2022.

Pia amesema amesema gharama za uingizaji wa mafuta katika bandari ya Dar es salaam , thamani ya shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani, gharama za usafiri , Bima na ‘Premium’hadi Zanzibar, kodi za Serikali , na kiwango cha faida kwa wauzaji wa Jumla na Reja Reja.

Akizitaja bei hizo amesema mafuta ya Petroli  kwa mwezi wa Machi yatakuwa 2,459. ambapo February ilikuwa 2,298. Diseli 2, 500 ambapo February ilikuwa2.345 na mafuta ya taa 1,811  ambapo February ilikuwa 1,890 .

Akitoa ufafanuzi amesema kupanda kwa bei za mafuta  kumechangia mgogoro wa uliopo Uambapo Urusi na Ukraine.

Aidha amesema mabadiliko hayo ya bei za mafuta yataanza rasmi kutumika kuanzia leo siku ya Jumatano ya tarehe 09/03/2022.

Zura inapenda kuwajuilisha wananchi kuwa bei zilizotangazwa ndio bei halali  na inawataka kudai risiti kila unaponunua 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.