Habari za Punde

Taasisi ya Zanzibar maisha Bora foundation (ZMBF) yasaidia wanawake na watoto Zanzibar

Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar maisha Bora foundation (ZMBF) dkt. Mwatima Abdalla Juma akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya wasichana Ben Bella Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae pia ni  mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi wakati walipofika skulini hapo kwa ajili ya kuwapatia  msaada wa taulo za kike wanafunzi wa Skuli hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya Taisisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) dkt Mwatima Abdalla Juma Akimkabidhi kwa niaba ya mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni mwenyekiti wa Taasisi hiyo mama Maryam Mwinyi box la taulo za kike rais wa Serikali ya wanafunzi Skuli ya wasichana BenBella Anna Adam Nuhu,wakati alipofika skulini hapo kwajili yakutoa msaada huo
Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation  dkt.Mwatima Abdalla Juma  Akimkabidhi Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae pia ni  mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi pempas Mkurugenzi Mkuu Hospital ya Mnazimmoja dkt.Marijan Msafiri  kwaajili ya watoto wanaozaliwa hospitalini hapo ikiwa ninmsaada kutoka Taasisi ya (ZMBF)

Mkurugenzi Mkuu Hospital ya Mnazimmoja Marjani Msafiri  akitoa neno la shukurani Kwa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation mara baada ya kupokea msaada wa pempas kwaajili ya watoto wanaozaliwa hospitalini hapo.

 

Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) dkt.Mwatima Abdalla Juma Akimkabidhi  Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae pia ni  mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi box la taulo za kike Mkuu wa wanafunzi wa kike Chuo cha Mafunzo Zanzibar SP Tunda Omari Kingalu  kwaajili ya wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Magereza  ikiwa mi msaada kutoka (ZMBF).

 

Mkurugenzi Taasisi ya wajane Zanzibar tabia makame akizungumza machache katika hafla ya makabidhiano ya msada wa taula za kike kutoka ZMBF kwa wagonja wa akili wakike waliopo katika Hospitali ya maradhi ya Akili Kidongo Chekundu Zanzibar.

 

Mjumbe wa Bodi ya Zanzibar maisha Bora Foundation (ZMBF) dkt.Mwatima Abdalla Juma  Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae pia ni  mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi Akimkabidhi mgonjwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital ya maradhi ya akili Kidongo Chekundu Maryam Hashim Abdalla Kwa ikiwa ni msaada kutoka ZMBF.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.