Habari za Punde

Ziara ya kutembelea miradi ya viungo Zanzibar kwa wakulima wadogo

Mkulima wa Bustani za nyumbani (kitchen garden) Maryam Juma Mcha wa Kijichi Magengeni akitoa ufafanuzi kuhusu Mboga ya Chaya ambayo anaipanda nyumbani kwake mara baada ya kupata elimu ya shamba darasa  kupitia mradi wa viungo,wakati alipotembelewa na watendaji wa mradi huo unaofadhiliwa na jumuiya ya Nchi za Ulaya kupitia programu ya Agri-connect kuangalia Maendeleo ya mradi na kusikiliza changamoto zinazomkabili .
Mkulima wa viungo Aviwa Ali Songora mkaazi  wa Kizimbani akielezea kuhusu kilimo cha  vanilla  anachoendelea kukilima mara baada ya kupata elimu   kutoka  kwa shamba darasa kupitia mradi wa viungo unaofadhiliwa na jumuiya ya Nchi za Ulaya kupitia programu ya Agri-connect wakati alipotembelewa na watendaji wa mradi huo kuangalia Maendeleo ya mradi,Bi Aviwa anamiliki shamba la ekari tatu Kizimbani  likiwa na mivanila 800 akikabiliwa na uhaba  wa maji ya kumwagilia.
Afisa kilimo katika mazao ya viungo Community Forest Pemba (CFP)Ali Said Juma  akitoa maelezo kuhusu lengo la mradi wa viungo unaofadhiliwa na jumuiya ya Nchi za Ulaya kupitia programu ya Agri-connect wakati wa ziara ya kuwatembelea wakulima wa shamba darasa kuangalia Maendeleo ya miradi na changamoto zinazowakabili, ziara hiyo  ilianzia Kwa wakulima wa Bustani za nyumbani (kitchen garden)Kijichi ,wakulima wa viungo Kizimbani na Kiboje Muembeshauri na kumalizikia shamba la mbogamboga Kivunge .

Mkulima wa shamba darasa Kiboje Mwembeshauri Jaribu Mwinyi Khamis akielezea kuhusu kilimo cha hiliki wakati alipotembelewa na watendaji wa mradi wa viungo unaofadhiliwa na jumuiya ya Nchi za Ulaya kupitia programu ya Agri-connect kwa lengo la  kuangalia Maendeleo ya mradi na kusikiliza changamoto zinazomkabili.

 


Mkulima wa bustani za nyumbani (kitchen garden)Salama Haji Juma mkaazi wa Kivunge akielezea faida anazozipata kutokana na kilimo hicho wakati alipotembelewa na watendaji wa mradi wa viungo kuangalia Maendeleo ya mradi na kusikiliza changamoto zinazomkabili,mradi wa viungo unafadhiliwa na jumuia ya Nchi za Ulaya kupitia programu ya Agri-connect.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.