AFISA Mdhamini Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mohamed Nassor Salim, akitoa taarifa ya
janga la moto lililotokea katika bweni la wanawake skuli ya Utaani Wete, kwa
mawaziri wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kamati ya ulinzi na usalama Mkoa,
walimu na wananchi
WAZIRI wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohamed Mussa, akizungumza katika hafla ya
kuwafariji wanafunzi ambao walipata mtihani wabweni lao kuungua moto hivi
karibuni, huko katika skuli ya utaani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
MKUU wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, akizungumza katika kikao cha kuwafariji
wanafunzi waliopata mtihani wabweni lao kuungua moto hivi karibuni, katika
kikao cha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
BAADHI ya wanafunzi
wa kidato cha sita ambao mwaka huu watafanya mitihani yao ya mwaka, wakiwa bado
na hudhuni juu ya kuteketea kwa moto vifaa vyao vilivyokuwemo ndani ya bweni la
wanawake skuli ya Utaani, wakati wakikao na waziri wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali huko Wete
WAZIRI wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Harusi Said Suleiman, akizungumza na
wanafunzi, walimu na wazazi wa wanafunzi waliopata na mtihani wa bweni lao
kuungua moto la skuli ya utaani hivi karibuni
MKURUGENZI wa Taasisi
Ya Ifraj Zanzibar Foundation Abdalla Said Abdalla, akizungumza katika hafla ya
kukabidhi vifaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 20, kwa uongozi
wa skuli ya utaani kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita ambao wanataraji
kufanya mitihani yao ya taifa, ambapo vifaa vyao viliteketea kwa moto
MWAKILISHI wa Bodi ya
Milele Zanzibar Foundation Ali Bakar Hamad, akizugumza katika hafla ya
kukabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 20, kwa wanafunzi wa kidato
cha tano hadi cha kwanza kwa skuli ya sekondari Utaani, ambao bweni lao
lilipata mtihani wakuungua moto hivi karibuni
AFISA Mdhamini Wizara
ya habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mafamau, akizungumza
katika hafla ya kuwafariji wanafunzi ambao bweni lao lilipata mtihani wakuungua
moto hivi karibuni.
AFISA Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim, akijadiliana jambo na watendaji kutoka Wizara hiyo wakati wa kikao cha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohamed Mussa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Harous Said Suleiman, walipofika kuwafariji wanafunzi wa skuli wa Utaali waliopata mtihani wabweni lao kuungua moto hivi karibuni.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment