Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,. Hemed Suleiman Afutarisha Wananchi wa Mkoa wa Mjini Unguja.

Viongozi na wananchi mbali mbali wamejumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar. 

Miongoni mwa waluohudhuria katika futari hiyo ni Naibu Waziri Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Ali Suleiman, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Matar Zahor Masoud, Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Thabit Idarou Faina, wakuu wa wilaya, Maafisa Wadhamini wa Wizara mbali mbali kisiwani Pemba, Viongozi wa Dini, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi mbali mbali.

 

Akitoa Shukurani kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Matar Zahor Masoud amewashukuru wananchi waliohudhuria katika futari hiyo kwa kuungana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kueleza kuwa lengo la futari hiyo ni kuwakutanisha wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba ili kuendeleza umoja na mshikamano. 

 

Aidha Mhe. Zahor amewataka wanachi wa Zanzibar kuungana na Serikali katika kupinga matendo ya udhalilishaji na kuwataka kuwa mabalozi wa kukemea matendo maovu yaliyomo katika jamii.

 

Pamoja na Mambo mengine amewakumbusha waumini hao kuchukua hatua za ziada katika kupiga vita madawa ya kulevya ambayo yanapoteza nguvu kazi ya Taifa 

 

Sambamba na hayo Mhe. Zahor amewaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 

Akitoa Shukurani kwa Niaba ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba Maalim Ali Bakari Haji amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuandaa futari hiyo ambayo inaonesha dhahiri Makamu wa Pili wa Rais kujiweka karibu na wananchi wa Zanzibar.


Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

15/04/2022   


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.