Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz
Said Ali akimkabidhi zawadi ya Ramadhan, Rashid Ali Mohamed ambaye ni mwandishi
wa habari wakati wa uzinduzi wa Ofay a Ramadhan kwa wateja wa Zantel. Ofa hiyo
inalenga kuwapa maudhui ya kiislam kama mafundisho,nasheed,adhana, dua na
kuwakumbusha muda wa futari na daku.
Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz
Said Ali (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
Ofa ya Ramadhan kwa wateja wa Zantel.Kulia ni Afisa wa Bidhaa, Edwin Byampanju.
Ofa hiyo inalenga kuwapa maudhui ya kiislam kama mafundisho,nasheed,adhana, dua
na kuwakumbusha muda wa futari na daku.
Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel leo imezindua ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo itawapa maudhui mbalimbali ya kiislamu yenye kuimarisha imani zao katika kipindi chote cha mwezi mtukufu kwa gharama nafuu.
Ofa hiyo ni sehemu ya azma ya Zantel ya kuhakikisha inakuwa karibu na wateja wake kwa kutoa suluhu zenye kuboresha maisha kijamii na kiuchumi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofa hiyo, Mkuu wa Fedha wa
Zantel, Aziz Said Ali alisema ofa hiyo ni mahususi kwaajili ya mwezi mtukufu na
kwamba imelenga kusogeza maudhui mbalimbali kwa watumiaji wa Zantel ili
kuwasaidia kuufanya mwezi mtukufu kuwa mkamilifu.
‘’Zantel inapenda kuwatakia
waislamu wote duniani mwezi mtukufu wa Ramadhan.Tunatambua mwezi huu ni muda
muafaka wa kuimarisha imani zetu kwa kufanya matendo yaliyo mema pamoja na kufanya
swala,” alisema na kuongeza;
“Zantel tumeona ipo haja ya kuungana na Waislamu wote hapa
nchini kwa kuleta huduma hii ya Ramadhan ambayo itawapa maudhui mbalimbali
yanayoendana na mwezi huu ili kukuza imani yetu pamoja na kuwakumbusha mida ya
swala tano za kila siku,” alisema.
Maudhui hayo ni pamoja na Dua, Qaswida za Ramadhan ‘Nasheed’,
Swala za Taraweeh pamoja na jumbe za sauti kuwakumbusha muda wa daku na Futari.
Ukijiunga na huduma hii utapata SMS tano za kukumbusha muda wa swala kwa siku.
Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko wa Zantel, Rukia Iddi Mtingwa
alisema wateja wanaweza kupata ofa hiyo kwa njia ya simu mahali popote jambo
litakalowasaidia kuwa imara kiimani muda wote.
“Lengo letu ni kuhakikisha huduma hii inamnufaisha kila mtu na ndio maana tumehakikisha inapatikana kwa gharama nafuu sana. Kwa Shilingi Mia moja tu (Tsh 100) kwa siku, mteja wetu ataweza kupata taarifa zote hii ambayo itamsaidia kutimiza ibada zake katika mwezi huu mtukufu.”
Ili kupata huduma hii mteja wa Zantel atapiga namba fupi ya 15582 na atafuata maelezo kisha Chagua Ofa ya Ramadhan.
No comments:
Post a Comment