Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Awasili Mkoani Dodoma leo 16-5-2022.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo tarehe 16 Mei 2022, amewasili Jijini Dodoma kwaajili ya Ufunguzi wa Wiki ya Kitaifa ya Ubunifu.

Katika uwanja wa Ndege wa Dodoma, Mheshimiwa Othman ambaye ameongozana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, amepokelewa na Viongozi mbalimbali wa  Serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama, wakiongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Faustine Mkenda.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman akiwa na Mkewe Mama Zainab Kombo Shaib na (kulia) Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Faustine Mkenda, wakielekea katika chumba cha mapumziko baada ya amewasili Jijini Dodoma kwaajili ya Ufunguzi wa Wiki ya Kitaifa ya Ubunifu.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Faustine Mkenda.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.