Habari za Punde

Maofisa Mipango Watakiwa Kutoa Sauti kwa Pamoja

Na.Takdir Suweid.

Maafisa mipango wametakiwa kufuata mpango mkuu wa Serikali ili kuweza kuwa na sauti ya pamoja.

Wito huo umetolewa na Kamishna wa idara ya mipango ya kitaifa , maendeleo ya kisekta na kupunguza umasikini Zanzibar Ndg.Siti Abasi Ali wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku 3 kwa maafisa mipango wa taasisi mbalimbali ikiwemo za mkoa wa mjini magharibi.

Amesema  mpango huo utasaidia kurahisisha maendeleo kwa wananchi kwani utakuwa na malengo yaliofanana.

Amewataka maafisa mipango hao kushirikiana na wizara ya nchi ofisi ya raisi fedha na mipango kupitia tume ya mipango ili kuweza kuielewa mipango ya serikali na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake dkt ramadhani khamis sosela ambae ni ni afisa muandamizi wa tume ya mipango Zanzibar amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa uelewa kwa maafisa hao na kuweza kuhuisha mipango ya kisekta ili iweze kuenda sambamba na maendeleo ya sekta zao.

Hata hivyo amewataka kushirikiana na kuwa kitu kimoja ili malengo yaliokusudiwa na serikali kuwapatia wananchi maendeleo ya haraka yaweze kufikiwa.

Mafunzo hayo ya siku 3 yamewashirikisha maafisa mipango wa mkoa wa mjini magharibi,wilaya na mabaraza ya manispaa yaliomo katika mkoa huo, wizara ya tamisemi,ofisi ya raisi na tume ya mipango ili kutoa elimu ya mipango ya kitaifa na kuondosha migongano iliokuwa inajitokeza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.