Habari za Punde

Alhaj Dk.Mwinyi Amesisitiza Juhudi za Makusudi Zitaendelea Kuchukuliwa Kuhakikisha Ahadi Kwa Wananchi Zinatelezwa.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na Wananchi wa Kijiji cha Fumba wakifuatilia hutuba ya Sala ya Ijumaa ikisomwa na Khatib Sheikh.Maulid Issa Shani(hayupo pichani)kabla ya Sala ya Ibada ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Fumba Bondeni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 17-6-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja baada ya kumalizika kwa Ibaada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Fumba Bondeni leo 17-6-2022.
WANANCHI wa Kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Fumba Bondeni leo 17-6-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh.Khamis Mussa Khamis (kushoto kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Fumba Bondeni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 17-6-2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kwamba juhudi za makusudi zitaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha ahadi zilizoahidiwa kwa wananchi zinatekelezwa ipasavyo.

Alhaj Dk. Mwinyi ameeleza hayo leo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya Sala ya Ijumaa huko katika Msikiti wa Ijumaa Fumba Bondeni, Wilaya ya Magharibi ‘B’, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika salamu zake hizo, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kuwa anaamini kwamba bado changamoto za kimaendeleo zipo lakini juhudi zitaendedea kuchukuliwa usiku na mchana na Serikali anayoiongoza katika kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.

Hivyo, Alhaj Dk. Mwinyi aliwanasihi waumini wote nchini kuendelea kuomba dua ili Mwenyezi Mungu aendelee kumpa nguvu kuweza kutekeleza yale aliyoyaahidi.

Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi aliwaahidi waumini wa Msikiti huo wa Ijumaa Fumba Bondeni kuzipatia ufumbuzi changamoto zao zinazowakabili ambazo walizitoa mbele yake ikiwemo huduma ya maji safi na salama.

Nae Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Mfaume aliwasisitiza waumini wote nchini kuendelea kumuombea dua Rais Dk. Mwinyi ili  aweze kutekeleza vyema majukumu yake kwani ana kazi kubwa ya kuwaongoza wananchi wa Zanzibar na kuwaletea maendeleo endelevu.

Sambamba na hayo, Sheikh Khalid aliwataka waumini kuhakikisha wanazitumia vyema ndimi zao kwani ni miongoni mwa viungo ambavyo kiongozi wa Waislamu Mtume Mohammad (S.A.W), amesisitiza vitumiwe vizuri ili kuepuka na adhabu za Mwenyezi Mungu huku akisisitiza kusema na kutenda yaliyomazuri.

Mapema akitoa hotuba ya Sala ya Ijumaa, Sheikh Maulid Issa Shani aliwanasihi waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kufanya mambo mema  kwani kila analofanya mja ninajulikana na linaandikwa na hatimae atalipwa kwa jema ama ovu alilolifanya.

Pamoja na hayo, Sheikh Maulid Issa Shani katika hotuba yake hiyo alieleza kwamba Mwenyezi Mungu atawalipa waja wake kutokana na amali zao walizozifanya duniani hivyo, alisisitiza haja ya kuendelea kutenda mambo mema na kuepukana na kutenda maovu.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano,

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.