Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, Bibi Fatma Karume akizungumza na Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakati alipomtembelea nyumbani
kwake Bumbwini Mkoa wa Kaskazini, Zanzibar. Wengine pichani kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na
Mratibu Mkuu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) – Dodoma
Bw. Khalid Bakar Hamran.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Abdallah Hassan Mitawi akizungumza na Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Shekhe Abeid Aman Karume, Bibi Fatma
Karume wakati wa ziara katika makazi yake Bumbwini Mkoa wa Kaskazini, Zanzibar.
Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Hayati Shekhe Abeid Aman Karume, Bibi Fatma Karume akisoma kitabu
cha Historia ya Muungano wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Bi. Mary Maganga na ujumbe wake katika makazi yake Bumbwini Mkoa wa Kaskazini,
Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga
akiagana na Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, Bibi Fatma Karume baada ya
kumtembelea na kufanya mazungumzo katika makazi yake Bumbwini Mkoa wa
Kaskazini, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment