Na Khadija Mgeni
Makarani wa sensa ya
watu na makaazi nchini wamewaomba viongozi mbalimbali waliopo kwenye kaya zao
kuzidi kutowa elimu juu ya sensa ya watu na makazi kwani ipo haja ya viongozi
wa kaya kutowa hamasa zaidi kwa wananchi wao.
Hayo yamesemwa na
makarani wakati wa mahojiano na wahamasishaji wa sensa kutoka
Afisi ya Mtakwimu Mkuu wakati walipofika kwenye ziara ya kuangaliya
mafunzo kwa vitendo katika kaya mbalimbali za Mkoa wa Mjini Magharibi
.
Aidha waliwasihi
viongonzi wa kaya hizo kutoa elimu kwa jamii iliyo wazunguka
kwa lengo la kufanikisha sensa hiyo .
Makarani hao
wamewasihi wananchi watakapofika katika kaya zao kuonesha ushirikiano mkubwa
kwa kuwapatia takwmu sahihi kwa maendeleo ya kaya zao ikiwemo elimu, afya,
majengo pamoja na miundombinu ya barabara.
Sambamba na hayo
wamewataka wananchi kutoa taarifa sahihi kwa wanakaya pale atakapopata dharura
ya kutokuwepo kwenye kaya yake.
Kwa upande wananchi wa
kaya zilizodadisiwa kwa njia ya mafunzo ya vitendo wamesema wako tayari
kushirikiana na makarani watakaopita katika kaya zao ili kuweza kuandaa mipango
mizuri ya taifa kwani bila ya takwimu sahihi huwezi kupata mipango ya
kimaendeleo kwa maslahi mapana ya nchi.
Pia wananchi hao
wameishukuru serikali yao kwa kuandaa kamati ya uhamasishaji ambayo imefanya
kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii na kuwasaidia kujuwa na kuondokana na dhana
potofu juu ya sensa.
Nae mratibu wa sensa
wilaya mjini ndugu Khamis Abdurahman Msham amewashukuru wanakaya kwa kuonesha
mashiriano yao ya dhati hali ambayo imewatia matumaini ya kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa sensa ya mwaka huu pia kwa upande wa makarani hao wameonesha uthubutu
mkubwa wa kufanya kazi kwa uweledi katika mafunzo kwa vitendo
sambambana na kutoa wito kwa wananchi kuwa tayari kuhesabiwa wakati
utakapo fika.
Tanzania kila baada ya
miaka kumi hufanya zoezi la sensa na watu na makazi ili kuweza kupata takwmu
sahihi kwa mipango ya maendele zimebaki takiribani siku kumi na moja kufikia
kwa sensa ya mwaka huu
No comments:
Post a Comment