Habari za Punde

Mhe Hemed afunga Kongamano la Nne la Nishati Tanzania

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefurahishwa na ushiriki wa Kampuni mbali mbali ya ndani na ya nje ya Tanzania katika Kongamano la Nishati lililofanyika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre Jijini Dar-es-salaam .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo akifunga Kongamano la Nne la Nishati Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre Jijini Dar-es-Salaam.

 Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka mipango madhubuti ya kuwavutia Wawekezaji katika Sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Nishati ambapo ushiriki wa Kampuni Thamanini na Tisa (89) katika Kongamano hilo kutoka Nchi mbali mbali   kumethibitisha utayari wa Kampuni  hizo kuja kuwekeza Tanzania.

Amesema miongoni mwa Mipango ya Serikali ni kuzingatia Maslahi ya wananchi pamoja na Wawekezaji ili kuinua Sekta ya Nishati na kukuza Uchumi wa Nchi.

Mhe. Hemed amesema Asilimia kubwa ya Wawekezaji wa Kampuni hizo ni Matunda ya Ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutembelea Nchi mbali mbali kwa kutafuta fursa za uwekezaji.

Mbali na Wawekezaji hao wa Sekta ya Nishati kuhudhuria katika Kongamano hilo wamepata Fursa ya kujionea maeneo mbali mbali ya Tanzania hatua ambayo itapelekea kufahamu Fursa nyenginezo zilizopo Nchini.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefurahishwa kuona Kampuni nyingi zinazalisha Bidhaa Bora zenye Viwango na zina Zataalamu  Wazawa hatua ambayo inatanua Wigo kwa kuitangaza Tanzania.

Mhe. Hemed ametumia Fursa hiyo kuwaeleza Washiriki wa Kongamano hilo kuwa Sekta ya Nishati ni miongoni mwa Sekta zilizotoa Nafasi nyingi za Ajira kwa Watanzania hatua ambayo imeisaidia Serikali kupunguza kutegemewa katika Ajira.

Aidha Mhe. Hemed ameeleza kufurahishwa kwake kuona Sekta Binfasi inashirikiana vya kutosha na Serikali katika kuinua Huduma za Nishati Nchini kwa lengo la kukuza Uchumi wa Tanzania

Nae Waziri wa Nishatu Tanzania Mhe. January Makamba ameeleza kuwa Washiriki wa Kongamano hilo wameahidi kuleta Mageuzi katika Sekta ya Nishati kwa lengo la Kukuza Uchumi.

Amesema Tanzania imekuwa kimaendeleo kwa ushirikiano uliopo baina ya Wizara za Serikali na Sekta Binafsi ikiwa ni Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzitaka  Wizara za Serikali kushirikiana na Sekta Binafsi katika kukuza Uchumi.

 

……………………

Abdulrahim Khamis

Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

04/08/2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.