Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmi Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Dk.Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita, alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja, kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa iliofanyika leo 12-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja kuhudhuria hafla ya Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa, iliyofanyika katika ukumbi huo leo 12-8-2022, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita na(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.
BAADHI ya Vijana na Wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 12-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga makofi kumpongea Kijana Neema Suri akitowa burudani ya muziki wa Alam (hayupo pichani) wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 12-8-2022 na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
WAZIRI Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 12-8-2022, kabla ya kumkaribia mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kuhutubia katika hafla hiyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa, maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 12-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya Picha Maalum Iliyotengenezwa na Vijana wa Zanzibar,  wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa, akikabidhiwa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita na (kulia kwa Waziri) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Vijana wa Mabaraza ya Vijana Zanzibar waliosimama nyuma baada ya kumalizika kwa hafla ya Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 12-8-2022.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.