Habari za Punde

Tabora na Kigoma Waibuka Mabingwa wa Kuruka Chini Michuano ya UMISSETA 2022

Na.Eleuteri Mangi

Mkoa wa Kigoma umefanikiwa kubeba Medali katika mchezo wa kuruka chini upande wa Wasichana, huku Mkoa wa Kigoma umebeba Medali kama hiyo upande wa Wavulana, katika Mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) mkoani Tabora.

Tabora imebeba Medali hiyo kupitia mwanafunzi Mwalu Madirisha aliyeruka umbali wa mita 4 kwa Sentimita 96, huku Mpaji Gibson wa Kigoma akiruka umbali wa mita 6 kwa Sentimita 34.

Mshindi wa pili upande wa Wavulana ni Elia Clement kutoka Arusha aliyeruka mita 6 kwa sentimita 17, huku msindi wa tatu ni Andrea Luhaga kutoa Mkoa wa Tabora aliyeruka mita 5 kwa sentimita 68.

Katika upande wa Wasichana, Mkoa wa Pwani umeibuka nafasi ya pili kupitia Elizabeth Keryaro aliyeruka mita 4 kwa sentimita 77, ambapo nafasi ya tatu imekwenda Tanga kupitia Hadija Ramadhani aliyeruka mita 4 kwa sentimita 73.

Mikoa mbalimbali iliyoshiriki mchezo huo ni pamoja na  Singida, Simiyu, Dar es Salaam , Katavi, Shinyanga, Geita, Arusha  na Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.