Habari za Punde

Arusha na Pwani Wabeba Medali Riadha Mita 1500 UMISSETA 2022

Na.Eleuteri Mangi

Katika Mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) mwaka 2022 yanayoendelea mkoani Tabora, Mkoa wa Arusha na Pwani wamekuwa Bingwa Riadha Mita 1500.

Mkoa wa Arusha umebeba Medali ya Ubingwa wa mita 1500 upande wa Wavulana kupitia mwanafunzi Damian Christian aliyekimbia kwa muda wa Dakika 4, sekunde 5 nukta 91.

Upande wa Wasichana, Mkoa wa Pwani umeibuka Bingwa kwenye mbio hizo kupitia mwanafunzi Salima  Charles aliyekimbia kwa muda wa Dakika 04, sekunde 40 nukta 64.

Aidha, Mkoa wa Mara umefanikiwa kuchukua nafasi ya pili na ya tatu, ambapo Nyanzobe Mbahi ameshika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa muda wa Dakika 4, sekunde 53 nukta 94, na nafasi ya tatu ikienda kwa Neema Nyaisawa aliyetumia Dakika 4, sekunde 55 nukta 28.

Katika upande wa Wavulana, Mkoa wa Manyara umekamata nafasi ya pili kupitia Agustino Leornad aliyekimbia kwa Dakika 4, sekunde 13 nukta 78; Na nafasi ya tatu imeenda Mkoa wa Geita kupitia mwanafunzi Jackson Charles aliyekimbia kwa muda wa Dakika 4, sekunde 17 nukta 68.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.