Habari za Punde

Ubunifu na Usafi Kivutio UMISSETA 2022

 

Na Shamimu Nyaki

Ubunifu, nidhamu na usafi ni sehemu ya mashindano Katika Mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) yanayoendelea  Mkoani Tabora ambapo washiriki ambao ni wanafunzi  wa shule za Sekondari hushiriki zoezi hilo kila asubuhi.

Mkoa wa Tabora ni mojawapo ya kivutio cha Ubunifu kwa bweni la wanafunzi wa kike kutoka mkoa huo kuchora Ranani ya Afrika Mashariki kwa kutumia kokoto Agosti 16, 2022.

Wanafunzi hao pia wametengeneza Bendera za nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, na kubuni ukumbi unaotumika kuendesha Mikutano ya Jumuiya hiyo.

Mkoa mwingine uliofanya vizuri ni Mkoa wa Mwanza, baada ya Wanafunzi hao kubuni hospitali pamoja na wodi ya kulaza wagonjwa, huku pia wakionesha mandhari na malighafi zinazopatikana katika mkoa huo.

Kwa upande wa Mkoa wa Arusha ulionesha ubunifu mzuri, ambapo Wanafunzi wamebuni sehemu za vivutio vya maporomoko ya maji pamoja na Msikiti unaotumiwana Waislam katika Ibada.

Mikoa mingine iliyoshiriki zoezi hilo ni Dodoma, Manyara na Morogoro.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.