Habari za Punde

Wanaodai Urais wa Samia si wa Kikatiba sio wakweli - Kinana

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akipokea matembezi ya wana CCM ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM)
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati akiwasili Afisi Kuu ya CCM, Mkoa wa Kaskani Unguja kulipofanyika kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.
Vijana wakifuatilia kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofanyika Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo. Katika kongamano hilo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, alikuwa mgeni rasmi
Vijana wakifuatilia kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofanyika Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo. Katika kongamano hilo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, alikuwa mgeni rasmi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kufanyika Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana  akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kufanyika Mahonda Wilaya ya Kaskazini B.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ameweka wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hasasan ni Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amepatikana kwa mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kupigiwa kura na wananchi.

Kinana ametoa ufafanuzi huo jana wakati akizungumza na wana CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kutekeleza vema Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020/2025.

“Nataka niseme na vizuri Watanzania wakajua tangu Rais Samia achukue uongozi wa taifa letu kuna kauli nimekuwa nikisikia baadhi ya kauli kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba. Kauli hii ina ukweli lakini haina ukweli.

“Inaukweli kweli kwasababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kila chama kitaweka mgombea na mgombe mwenza na Katiba inasema mgombea Mwenza na mgombea wanafasi moja ya kupiga kampeni ya chama chao na kila Chama kinapochagua Mgombea Mwenza,”alisema Kinana.

Alifafanua CCM hakimchagua mgombea mwenza kwa kucheza bahati nasibu ya kutumbukiza halafu tuangalie nani kapata nani kakosa bali wameweka sifa, kwa kuangalia uwezo, kukubalika , anafaa ,uwezo wa kufanya kampeni, , anaweza kuleta kura nyingi na mwisho wanajiuliza iwapo mgombea kwa sababu yoyote atakuwa hayupo au ameondoka madarakani je mgombea mwenza atamudu nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vigezo vyote hivyo vilipimwa kwa Samia.

“Anaweza ndio , ana mudu, ndio, anajua kazi yake ndio, anaweza kufanya kampeni ndio, anaweza kumsaidia mgombea na kuleta kura ndio. Mwisho iwapo mgombea kwasababu yoyote ataondoka madarakani kwa njia za kidunia au zake Mwenyezi mungu anaweza kuchukua nafasi hiyo wana CCM tukajiridhisha ndio anaweza.

“Kwa hiyo kwa wale wanaosema huyu ni Rais wa Katiba si kweli , Rais Samia Suluhu Hassan alipimwa kabla ya kupewa hiyo nafasi, bahati nzuri mimi nilikuwa Katibu Mkuu wa Chama, nilishiriki vikao vya awali mwaka 2015 na wengine walikuwepo kwenye vikao, hayo maswali yote tulupojiuliza tukasema anaweza ,ana mudu hiyo kazi, anaongeza kura, ana uzoefu, anakifahamu chama cha mapinduzi lakini kama anahitajika kuwa Rais anaweza.

“Sasa unaposema Rais Samia ni Rais wa Katiba hakuchaguliwa sio kweli lakini kubwa zaidi Rais anapopigiwa kura na mgombea mwenza anapigiwa kura na kabla haijafika muda wa kupiga kura iwapo mgombea mwenza Mwenyezi Mungu atamchukua uchaguzi utasimmamishwa.”

Aliongeza kwa kueleza “Kwa nini usimamishwe? Kama kweli yeye ni Rais tu wa Katiba tuendeee kupiga kura mambo yaishe .Mwaka 2005 tulikuwa na mgombea mwenza wa CHADEMA Jumbe Rajab Jumbe mwenyezi Mungu akamchukua , uchaguzi ulisimamishwa, kwanini ulismamishwa? Kwasababu na yeye ananafasi muhimu hawezi rais wan chi akapigiwa kura au mgombea akapigiwa kura kama mgombea mwenza hayupo.

"Wanasema Rais Samia ni Rais wa Katiba hawasemi kweli, Rais Samia ni Rais aliyetokana na mchakato wa uchaguzi , alipopigiwa kura Rais Magufuli na Samia alipigiwa kura hapo hapo kama rais aliyemtangulia angekuwa ameondoka madarakani kwa kujiuzulu au kwasababu nyingine yoyote angekuwa Rais lakini kwasababu za Mwenyezi Mungu Rais Samia amechukua dhamana.

"Kwanini basi uchaguzi wa Chadema mwaka 2005 ulisimamishwa? Kwasababu wote wawili wanatokana na utaratibu wa Katiba uliowekwa kwa hiyo Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wale wanaosema ni Rais wa Katiba wana ajenda yao, msiwasikilize. Kama hawajui au wanajifanya hawajui , nadhani sasa watajua, nilisema wanaosema Rais Samia ni wa Katiba hawasemi kweli na nimetoa maelezo.

"Sasa nitoe upande wa pili kweli ni Rais wa Katiba.Katiba inasema hivi kila Chama kitateua mgombea na mgombea mwenza, kwa hiyo kila Chama kinateua Mgombea na Mgombea Mwenza , Rais au mgombea anatokana na matakwa ya Katiba ya Jamhurii ya Muungano wa Tanzania.

"Mgombea mwenza ni matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano , kwa hiyo anateuliwa Samia kuwa mgombea mwenza ambaye baadae anakuwa Rais anatokana na matakwa ya Katiba kwa hiyo Rais Maguli ni Rais wa Katiba , unapendekezwa na chama chako, uakwenda kwa wananchi lakini hupigiwi kura peke yako unapigiwa na mgombea mwenza.

"Iwapo hayupo uchaguz unaahirishwa , kwa hiyo nimalize kwa kusema tukisema kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba husemi ukweli, Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.nchi ya Marekani Rais wa sasa ni Rais wa 46 , katika marais 46 waliowahi kufariki kabla ya muda wao walikuwa marais wa nane baadae wakachukua wagombea wenza ambao baadae wakaja kuwa marais," alifafanua.

Aliongeza kuwa, pamoja na hayo nchini Marekani hawajawahi kuwaita Marais hao ni WA katiba, "lakini hapa Tanzania wanaotaka kukoroga mambo wanakwambia Rais Samia ni Rais wa Katiba."

Katika hatua nyingine, Kinana alifafanua kuwa, katika kudhirisha sifa za uongozi wa Rais Samia ameweka alama kubwa za maendeleo katika kila mkoa wilaya na shehia nchi nzima.

"Yote haya ya mefanyika katika muda mfupi wa mwaka mmoja wa uongozi wake
fedha za maendeleo zimetokana na ukusanyaji mkubwa wa kodi kwa njia ya hiyari, fedha za misaada na mikopo zilikuja kotokana na kukubalika kwake duniani.


Kwa upande wake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, tikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameweka wazi kwamba kwa kazi nzuri anayoifanya Rais Samia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwatumikia na kuwaheshimisha Watanzania, kuiheshimisha Afrika na Dunia awataendelea kuwa madarakani hadi 2030.

Alisema kwa pamoja wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kusimamia maendeleo endelevu na kudumisha na kuimarisha muungano.

“Mitano kwa Rais Samia haina mjadala biashara imekwisha, kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu, Katiba yetu na utamaduni wetu huu mjadala haupo tena.Kama kuna mtu ana ndoto, hizo ndoto zikae pembeni Dk.Mwinyi tunamalizana 2030 , Chama hiki kina msingi na msingi wake mkuu ni Katiba, Kanuni na taratibu lakini kina utamaduni wake , hivyo viongozi hawa watatuvusha mpaka 2030 halafu ndio tunaangalia Katiba inasemaje.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.