Habari za Punde

Bilioni 27 Kujenga Bwawa la Kilimo cha Umwagiliaji Msagali Mpwapwa Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akimkabidhi Kablasha Mwakilishi wa Kampuni wa GNMS Contractors  Mhandishi Emmanuel Mponda itakayojenga bwala litakalotumika kwa Kilimo cha Umwagiliajia Msagali.

Na ,Mwandishi Wetu - Mpwapwa

KWA MARA NYIGINE TENA; Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo, imekabidhi rasmi kwa makandarasi GNMS Contractors eneo la Ujenzi wa Bwawa litakalotumika kwa kilimo cha Umwagiliaji litakalojengwa kwa thamani ya shilingi Bilioni 27.   

Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Dodoma Raphael Laizer amesema wakati wa makabidhiano ya eneo hilo la umwagiliaji jana jioni kuwa,

Bwawa hilo litakalokuwa na ujazo wa lita milioni tisini, litapelekea kuendelezwa kwa eneo litakalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta elfu tatu na mia tano (3500), ambapo ujenzi wa bwawa hilo unaotegemewa kuchukua miezi kumi na nane, utahusisha eneo ya unyweshwaji maji mifugo, matumizi ya binadamu na shughuli nyingine za kimaendeleo.

Awali, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kusaidia kundi hili maalum la wakulima, wavuvi na wafugaji na kumuasa mkandarasi na wasimamizi wote wa mradi huu kufanya kazi hii kwa weledi na kwenda na wakati.

Kwa Upande wake Mwananchi kwa kata ya Chunyu, Bi Easther Zeavela alitoa ombi kwa mkuu wa mkoa kuwaasa wasimamizi wa miradi inayokwenda vijijini kuwa makini, kwani mradi mingi inakosa usimamizi mzuri. “Uongozi wa juu unapoleta miradi huku vijijini, wasimamizi wasimamie vizuri ili pesa za miradi zitosheleze, mambo mengi tunaona yanaanzishwa na hayakamiliki.” Alisema mwananchi huyo

Ujenzi wa bwawa la msagali unaelezwa kuleta mafanikio mengi pindi utakapokamilika kutokana na asili ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko ya maramara, hivyo kingo za bwawa hilo linaweza kustiri miondombinu mingine kama vile ya marabara na umeme.

Mradi wa Bwawa la Msagali ni moja kati ya miradi 21 ya kilimo cha Umwagiliaji iliyosainiwa mbele ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya mwaka huu.

Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Dodoma Raphael Laizer akizungumza wakati wa kukabidhi Mradi wa bwawa la Umwagiliaji Msagali, Wilayani Mpwapwa, kulia ni mwakilishi wa kampuni ya GNMS Contractors itakayofanya kazi ya ujenzi wa bwawa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiongea wakati wa kukabidhi mradi wa Ujenzi la bwawa la Msagali wilayani Mpwapwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat Maganga akizungumza na wananchi wa kata ya Chunyu na Ng'ambi wilayani humo baada ya kukabidhi eneo la ujenzi wa mradi wa Bwawa la umwagiliaji.
Wananchi wa kata ya Ng'ambi na Chunyu katika mkutano wa  hadhara na viongozi wa Mkoa wa Dodoma.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.