Habari za Punde

Rais Dk.Hussein Mwinyi Aipongeza Cuba Kwa Kuendeleza Ushirikiano wa Muda Mrefu Kupitia Sekta ya Elimu na Afya

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 1-9-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania Yordenis Despaigne, aliefika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.

Rais Dk. Mwinyi aliishukuru Cuba kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kupitia sekta za elimu na  afya.

Alisema Taifa hilo limekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Zanzibar kutokana na msukumo mkubwa inayotoa kupitia sekta za Afya na Elimu, ambapo pamoja na kutoa msaada wa madaktari pia hutoa fursa za masomo kwa Wanafunzi wa Zanzibar.

Dk.Mwinyi alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar inahitaji kuongeza uwezo wake katika utoaji wa huduma za Afya kwa kuwa na madaktari na Manesi baada ya Serikali kujenga Hospitali 10 kutoka katika kila  Wilaya na hivyo akabainisha umuhimu wa kupata fursa za mafunzo.

Aidha, Dk. Mwinyi  alisema Zanziabr itaendeleza uhusiano na ushirikiano  uliopo kati yake na Cuba katika masuala mbali mbali ya kimataifa.

Nae, Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Yordenis Despaigne alisema Cuba inajivunia uhusiano na ushirikiano wa Kihistora kati yake na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, na kuahidi kuuendeleza, ili kusaidia juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma na kuimarisha  uchumi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Cuba Nchini Tanzania.Mhe. Yordenis Despaigne, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 1-9-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar mgeni wake Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa  zawadi ya picha na  mgeni wake Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.