Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Ziarani Pemba Atembelea Miradi ya Maendeleo

Na.Ali Moh’d . OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wakandarasi wanaojenga matangi ya maji kuongeza kasi ili kuendana na muda waliokubaliana katika mikataba.

Mhe. Hemed ameeleza hayo katika ziara ya kukagua miaradi ya ujenzi wa matangi MATANO ya maji  yenye uwezo wa ujazo tofauti  inayojengwa kwa pesa za ahueni ya uviko 19 kwa mikoa miwili ya pemba.

Ameeleza kuwa  serikali ya hitaongeza muda wa ujenzi wa miradi hio kinyume na makubaliano ambayo yamekubalianwa kwenye mkataba husika hivyo serikali haitavumilia ucheleweshaji wowote ambao utafanywa na mkandarasi anaejenga mradi waserikali kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Amesema serikali imejipanga kutatua changamoto ya upatiakananji wa maji safi na salama kwa unguja na pemba hivyo ni vyema wakandarasi kuongeza kasi katika ujenzi ili kuhakikisha serikali inafikia malengo iliyojiwekea kwa wananchi wake.

Mhe. Hemed amesema kuwa serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt. Hussein mwinyi haitapokea tangi lolote lililochini ya kiwango hivyo amemtaka mshauri elekezi kusimamia vyema ili kuhakikisha matangi hayo yanajengwa kwa kiwango na yanamalizika kwa wakati uliopangwa.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameutaka uongozi wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini kupitia Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha linachimba visima na kusambaza mabomba mapema ili yatakapokamilika matangi hayo yaweze kutumika mara moja.

“nivyema kuchimba visima mapema pamoja na kusambaza mabomba ya maji ili matangi yakimalizika tu yaweze kutumika na sio tukasubiri mpaka matangi yakamalizika ndio tukaanza kuchimba visima na kusambaza mabomba hii sio sawa wananchi wanashida sana ya maji”amesema

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameutaka uongozi wa ZAWA kuhakikisha mabomba yaliyopo bandarini yanafika sehemu husika ili yaweze kusambazwa maeneo yaliyokusudiwa.

Nae mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) dokta Salha Mohamed Kassim amesema miradi inayojengwa ni utekelezaji wa ahadi ya mheshimiwa rais kwa wananchi wake ya kuwaondolea changamoto zote hasa suala la upatikanaji wa maji safi na salama kwa unguja na pemba

Aidha dokta Salha amesema kuwa Wizara kupitia Mamlaka ya maji ZAWA itahakikisha inasimamia miradi yote inayojengwa na serikali ikiwemo hii ya pesa za ahuweni za UVIKO 19 inajengwa kwa viwango na kumalizika kwa wakati  kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais ametembelea vituo vya ununuzi wa zao la karafuu na kuuagiza uongozi wa wizara ya BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA kuimarisha miundombinu muhimu  kwenye vituo hivyo ikiwemo upatikanaji na Umeme wa uhakika.

Mhe. Hemed amesema kuwa suala la upatikanaji wa huduma bora kwenye vituo hivyo litasaidia kuondosha malalamiko yasiokuwa na tija kwa wakulima.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais ameiagiza wizara ya biashara na maendeleo ya viwanda kushirikiana na wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoa elimu kwa wakulima ili kulima kilimo cha kisasa ikiwemo kilimo cha mikarafuu.

Mhe. Hemed amesema kuwa serikali inathamini sana kilimo cha mikarafuu kwani ndio zao kuu ndani ya visiwa vya Zanzibar ukilinganisha na nchi jirani zianazolima zao hilo.

Hivyo amewataka wakulima wa zao hilo kuuza  bidhaa hio kwenye shirika la Taifa la biashara la (ZSTC) kwa maslahi ya taifa na kuepukana na walanguzi au kuuza kimagendo nje ya nchi amabapo itapelekea nchi kupata hasara.-

Amesema Serikali imejipanga kutoa mikopo kwa wakulima ili waweze kupata nyenzo bora na kuondosha changamoto zote zinazowakabili wakulima kwa maslahi ya taifa.

Sambamba na hayo makamu wa pili wa rais amelitaka shirika la Tifa la Biashara ZSTC kuweka mashine za kisasa kwenye vituo hivyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wakulima

Pia Mhe. Hemed amewataka wakulima kulinda hadhi ya zao hilo kwa kuimarisha usafi kwenye mashamba yao ili kupata karafuu yenye kiwango cha juu.

“Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na dokta Mwinyi imejipanga kuliboresha zao hilo siku hadi siku kwa maslahi ya wakulima na wazanzibari kwa ujumla”. 

Kwa upande wake waziri wa BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA Mhe. Omar Said Shaaban amesema kuwa Wizara imejipanga kuzitatua changamoto zote zinazowakabili wakulima wa zao la karafuu ili waweze kunufaika na zao hilo.

Mhe.Omar  amesema wizara imeweka madaraja kwenye zao hilo ili kuleta ushindani kwa wakulima na kuwaahidi wakulima hao kuwa wizara itahakikisha kuwa msimu ujao wa karafuu inaweka mashine za kisasa za kupimia zao hilo kila kwenye vituo vya uuzaji wa karafuu kwa lengo la kuwarahisishia wakulima kuuza bidhaa hiyo. 

Nao wakulima wa karafuu kisiwani pemba wameiomba serikali kuwatatulia changamoto zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu, kupandishiwa kwa bei zao hilo, pamoja na kubadilishiwa mashine za upimaji kwani zilizopo sasa ni za muda mrefu ili na hazileti usawa katika upimaji. 

Vile vile Katika ziara hiyo mhe. Hemed alipata fursa ya kutembelea ujenzi wa kiwanda cha mwani kinachojengwa eneo la Chamanangwe  mkoa wa Kaskazini Pemba na makandarasi mzawa kikosi cha kuzuia magendo KMKM ambapo ameutaka uongozi wa kikosi hicho kujenga kwa kiwango na kumaliza kwa wakati  kulingana na mkataba.

Mhe. Hemed amesema serikali italiongezezea thamani zao la mwani kwa kusindika na kusarifu ili kukidhi viwango vya kimataifa .

Nae mkurugenzi wa kiwanda cha mwani Dkt. Masoud Rashid Mohamed amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu kiasi cha shilingi  bilioni 8.2 kwa hatua ya mwanzo na kinatarajiwa kuzalisha tani elfu 30 kwa mwaka. 

kwa upande  mkandarasi wa ujenzi huo mkuu wa kikosi cha KMKM zanzibar KOMODOO Azana Hassan Msingiri amemuhahikishia makamu wa pili wa rais kuwa kwa kushirikiana na wakala wa majengo ZBA kikosi kitahakikisha kinajenga kiwanda hicho kwa ubora uliokusudiwa na kumalizika kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza.

Katika ziara hio makamu wa pili wa rais ametembelea ujenzi wa matangi ya maji Chanjaani, Kendwa, Pujini, Raha Wete, Kipange Konde na Kilindini Michweni  pia ametembelea vituo vya ununuzi wa karafuu Chonga naWete pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda cha Mwani Chamanangwe.

OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS

1.09.2022

Ali Moh’d

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.