Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zanzibar ‘Nuru Foundation’ ambaye pia ni mke wa Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib akiwa katika picha ya pamoja na Watoto Yatima wakati alipotembelea na kugawa msaada kwa
watoto hao huko Skuli ya Donge Mchangani leo Tarehe 11.09.2022. Picha na Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zanzibar ‘Nuru Foundation’ ambaye pia ni mke wa Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib akizungumza na Wazazi wa Watoto Yatima wakati alipotembelea na kugawa msaada
huko Skuli ya Donge Mchangani leo Tarehe 11.09.2022. Picha na Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zanzibar ‘Nuru Foundation’ ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib akimuuliza hali Bi Mboja Machono
Ali wa Kijiji cha Kandwi Kaskazini A
Unguja akiwa amembeba mtoto wake Asya
Kheir Ali . Bimboni ni miongoni wa wanakijiji hicho wanaoishi katika mazingira magumu. Mama
Zainab alikuwa na ziara ya kutembelea watoto yatima na wanawake wanaoishi
katika mazingira magumu huko Kaskazini Leo tarehe 11.09.22 . Picha na Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zanzibar ‘Nuru Foundation’ ambaye pia ni mke wa Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib akiwa amembeba mtoto Asya Kheir Ali
wa Kijiji Cha Kandwi Kaskazini A’ Unguja ambaye wawazi wake wanaishi katika
mazingira magumu. Mama Zainab alikuwa na ziara ya kutembelea watoto yatima na
wanawake wanaoishi katika mazingira magumu huko Kaskazini Leo tarehe 11.09.22 .
Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zanzibar Nuru Foundation Mama Zainab Kombo Shaib, ameikumbusha
jamii kuondoa dhana kwamba watoto yatima ni mzigo na lazima kutambua kwamba upo
wajibu wa kuwalea kwa pamoja na kuwapa kila aina ya matunzo wanayostahiki
ikiwemo elimu.
Mama Zainab
ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo
huko Donge Mchangani Kaskazini ‘A’
Unguja alipokuwa akigawa msaada chakula kwa watoto yatima na wanawake wanaoishi katika Mazingira Magumu
wilayani humo.
Amefahamisha
kwamba kwamba kufanya hivyo ni hatua muhimu ya kuwafanya watoto waliofiwa na
wazazi wao kuishi kwa furaha na kuendelea kupata matunzo na huduma mbali mbali
kutoka kwa jamiii.
Amesema
kwamba jumuiya ya Nuru Foundation inayojishughulisha na kuwasaidia mayatima na
wanawake waliokwenye mazingira magumu na kwamba pia ni wajibu wa kila mmoja
katika jamii kutimiza wajibu wa kuelemishana katika kuwatunza na kuthamini
watoto mayatima.
Mama Zainab
amewataka wazazi na walezi wenye watoto mayatima kuhakikisha kwamba hawabaki
nao majumbani kimya kimya na badala yake kuwasajili na kuwatolea taarifa zao kwa usahihi katika
taasisi na jumuiya za namna hiyo ili iwe rahisi kuwapatiwa misaada ya mahitaji
yao.
Ameonya
tabia ya baadhi ya wanawake kujisahau na kuwapoa manyanyaso watoto yatima
baadala ya kuwapatia haki zao ikiwemo elimu, makazi na nyenginezo za msingi ili
maisha yao yaweze kuwa bora.
Naye Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma
amesema kwamba watoto mayatima ni kundi kubwa lililopo ndani ya jamii linalohitaji kusaidiwa hivyo jumuiya ya Nuru
Foundation inafanya jambo jema kuisaidia serikali katika kuwapatia huduma watoto
wa aina hiyo.
Amefahamisha
kwamba hatua ya kuwasaidia watoto hao ni muhimu kuendelea kufanyiaka kwa kuwa
ni kuunga mkono juhudi za serikali kwa vile pekee haiwezi kufanya kila kitu .
Naye Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Bi Abeda
Rashid Abdalla, amesema kwamba shughuli za taasisi kama Nuru Foundation ni
muhimu hasa katika kuwasaidia kuwapunguzia mzigo wanawake ambao ndio wanaobeba
jukumu kubwa la kuwalea mayatima.
Kwa upande
wake Mratibu wa Watoto mayatima wa Mko awa Kaskazini Unguja Mwajuma Kali Makame
ameshukuru ujiyo wa Viongozi wa Jumiya hiyo ulioambatana na Uongozi wa Wizara
ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto na kusema kwamba inatoa fikra mpya
katika kuendelea na jitihada za pamoja ya kuwatunza na kuwalea watoto yatima na
wanawake wenye mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment