Habari za Punde

Juhudi mbali mbali zinafanywa kupunguza ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira Zanzibar – Mhe. Soraga

Na. Mwandishi Wetu ARKUU 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga wakati akijibu swali la Mheshimiwa Bakar Hamad Bakar Mwakilishi wa Wananchi Jimbo la Wawi juu ya upatikanaji wa takwimu sahihi za vijana wasiokuwa na ajira Zanzibar, katika vikao vya Baraza la kumi la Wawakilishi vinavyoendeleo huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

 

Amesema ni kweli kunakuwa na takwimu tofauti za vijana wasiokuwa na ajira nchini kutegemeana na chanzo cha takwimu hizo bali takwimu sahihi zinapatikana katika Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ambapo kwa mujibu wa takwimu za Utafiti wa ‘Intergrated Labour Force Survey’wa mwaka 2020/2021 idadi ya vijana wasiokuwa na ajira ni 109,868 sawa na asilimia 27.4 kutoka asilimia 21.3 kwa mwaka 2014

 

Amefahamisha kuwa kulingana na takwimu hizo kiwango cha ongezeko la vijana

wasiokuwa na ajira kimefikia asilimia 6.1 huku serikalim ikifanya juhudi mbali mbali ya kupunguza ogezeko hilo ikiwemo utoaji wa mikopo ya fedha za ahueni ya Uviko-19 kwa wajasiriamali, ujenzi wa vituo vya kulea wajasiriamali(Incubators) pamoja na program ya kuwajengea uwezo vijana waiotambulika na mfumo rasmi wa elimu (NEET) pamoja na program ya kuwawezesha vijana kupataka mfunzo katika sekta ya utalii kwa kushirikiana na chuo cha utalii kilichopo Maruhubi Unguja.

“Hii takwmi imeongozeka kutokana na changamoto ya janga la Uviko 19 lililoikuba dunia lakini tunaamini kupitia mikakati hii tutawawezesha vijana kupata ujuzi mbali mbali ili waweze kujiajiri na kuajirika.” Alisema Soraga

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.