Habari za Punde

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Timu ya KMKM Yakubali Kipigo cha Bao 2-0 Dhidi ya Timu ya Al Ahly Tripoli

Mshambuliaji wa Timu ya KMKM akimiliki mpira wakati wa mchezo wa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar, beki wa Timu ya Al Ahly Tripol akijiandaa kumzuia, Katika mchezo huo Timu ya Al Alhy Tripoli imeshinda mchezo huo kwa bao 2-0. 
Mchezaji wa Timu ya Al Ahly  akijianda kumpita beki wa Timu ya KMKM wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.Timu ya Al Ahly Tripol imeshinda mchezo huo kwa bao 2-0.

Kocha Mkuu wa Timu ya KMKM Hemed Moroco akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar baada ya kumalizika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar Timu ya KMKM imekubali kichapo cha bao 2-0, dhidi ya Timu ya Al Ahly Tripol.

Kocha Mkuu wa Timu ya Al Ahly Tripol Shirif akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar baada ya kumalizika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar Timu yake imefanikiwa kushinda mchezo huo dhidi ya Timu ya KMKM  kwa kuichapa  bao 2-0.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.