Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Balozi wa Australia Nchini Tanzania

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Balozi wa Austiralia Mhe.Luke Williams katika Nchi za Kenya,Rwanda na Tanzania,pia anawakilisha nchi yake Somalia na Burundi, leo wakati wa mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Austiralia Mhe.Luke Williams (katikati), katika Nchi za Kenya,Rwanda na Tanzania,pia anawakilisha nchi yake Somalia na Burundi wakati wa mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Jijini Zanzibar akiwa na ujumbe.
 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akibadilishdna mawazo na geni wake Balozi wa Austiralia Mhe.Luke Williams  katika Nchi za Kenya,Rwanda na Tanzania,pia anawakilisha nchi yake Somalia na Burundi, mara baada ya mazungumzo leo alipofika Ikulu Jijini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akibadilishdna mawazo na mgeni wake Balozi wa Austiralia Mhe.Luke Williams  katika Nchi za Kenya,Rwanda na Tanzania,pia anawakilisha nchi yake Somalia na Burundi, mara baada ya mazungumzo leo alipofika Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu]

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar  itaendeleza uhusiano na ushirikano uliopo kati yake na Australia kwa maslahi ya nchi mbili hizo.

Dk.Mwinyi amesema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams, ambae pia anaziwakilisha nchi za Kenya, Rwanda, Somalia na Burundi, ambapo amefika kwa ajili ya kujitambulisha.

Alisema kuna umuhimu kwa nchi mbili hizo kuendeleza ushirikiano uliopo wakati huu Zanzibar ikiweka kipaumbele katika kuimarisha uchumi wake kupitia Sekta za Uchumi wa Buluu, unaohusisha sekta za Utalii, kilimo cha mwani na Uvuvi.

Dk. Mwinyi alitumia fursa kuiomba Autralia kusaidia uimarishaji wa sekta hizo na kumpongeza Balozi huyo kwa dhamira yake ya kusaidia Zanzibar katika sekta ya kilimo.

Nae, Balozi wa Australia nchini Tanzania, Luke Williams aliahidi kuendeleza  ushirikano uliopo kati ya Australia na Tanzania pamoja na kuunga mkono azma ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya Uchumi wa Buluu kwa kuzingatia uwepo wa fursa mbali mbali.

Alisema Zanzibar ni kituo muhimu cha utalii kutokana na historia yake, kuwa na  mandhari ya kuvutia pamoja na Utamaduni wa watu wake.

Alimhakikisha Rais Dk. Mwinyi kuwa atafanya juhudi kusaidia  uendelezaji wa kilimo  kwa kuzingatia Zanzibar ina utajiri katika uzalishaji wa viungo.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.