Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar
akizungumza wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo leo
Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa Mabadiliko
ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam
ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza
na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa Mabadiliko
ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam
ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza
na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito kwa mataifa duniani kushirikiana katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa Mabadiliko
ya Tabianchi na Maendeleo ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano
na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Dkt. Jafo
alisema Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani
inakabaliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Alisema changamoto hizo zinaathitri uzalishaji
wa chakula unaosababishwa na ukame na mafuriko ya kudumu, uharibifu wa
miundombinu, uharibifu wa ardhi, uchakavu wa vyanzo vya maji, upotevu wa maji.
ya viumbe hai, viumbe vamizi, uhamiaji na mlipuko wa magonjwa.
Hivyo, Waziri Jafo alisema kutokana na
athari hizo, Tanzania inatumia wastani wa Dola za Kimarekani milioni 500 kwa
mwaka katika kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo.
“Katika Mkutano tutaweza kujadiliana na wenzetu kutoka
mataifa mbalimbali duniani kuhusu changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na
namna ya kupata fedha za zitakazotumika katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya
tabianchi,” alisema.
Aidha, Dk. Jafo
alibainisha kuwa Tanzania iliazimia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kati
ya asilimia 30 hadi 35 ikilinganishwa na mazingira ya Biashara ya hewa ya ukaa ifikapo
mwaka 2030, ambapo takriban tani milioni 138 hadi 153 za hewa hiyo zinatarajiwa
kupungua.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza Mhe.
David Concar alisema Mkutano huo ni jukwaa muhimu la kuzikutanisha nchi
mbalimbali kujadili namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mhe. Concar alisema kutokana na makubaliano
yaliyofikiwa kuwa nchi zinazoendelea kuchangia katika mapambano hya mabadiliko
ya tabianchi katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) uliofanyika
Glasgow, Scotland ni wakati sasa wa kutekeleza maazimio hayo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais Dkt. Omar Dadi Shajak alisema maeneo 143 ya Visiwia vya
Zanzibar yameathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kwa kuingiliwa na majichumvi
kutoka baharini.
Alisema kutokana na changamoto hiyo kilimo cha
mpunga kimeathiriwa na athari za mabadiliko ya tabianchi hali iliyosababisha
uzalishaji wa mpunga kupungua kwa kiasi kikubwa.
Hivyo, Dkt. Shajak alisema Mkutano huo utasaidia
kuweka mikakati endelevu ikiwemo kutafuta njia mbadala wa kukabiliana na athari
za mabadiliko ya tabianchi.
No comments:
Post a Comment