Na.Mwanajuma Abdi -Dar es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeri rasmi katika kongamano la Nishati safi ya Kupikia litalofanyika Novemba Mosi na Pili mwaka huu ili kupunguza vifo vinavyotokana na mfumo wa kupumua hususani wanawake.
Amesema
kongamano hilo litazungumzia hali ya sasa ya matumizi ya nishati ya kupikia na
ufahamu wake, kubadilishana uzoefu na fursa zilizopo pamoja na changamoto kwa
kutumia sera, sheria na masuala ya kodi katika kufikia matumizi salama ya
nishati.
Akizungumza
na wandishi wa Habari jana, Dar es Salaam Waziri wa Nishati Januaruy Makamba
amesema kongamano hilo litawashirikisha wadau kutoka serikalini na sekta
binafsi, litafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Alisema watanzania 33,000 wanakufa kwa mwaka, kutokana na
magonjwa ya kupumua kutokana na hewa ya
sumu wanayoimeza katika mapafu yao inayotokana na moshi wakati wa kupika
chakula kwa kutumia kuni na mkaa.
Alisema
athari ni kubwa kwa akinamama na watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano,
ambao mara nyingi huathirika wakati wa wanapopika,
hivyo moshi wa nishati hizo huwaathiri
kiafya.
Alieleza asilimia
72 ya nishati yote nchini inatumika kwa kupikia majumbani, ambapo asilimia nane
ya watanzania ndio wanaotumia nishati safi isiyotoa moshi, huku asilimia 63.5 ni nishati kwa kutumiua kuni na asilimiza
zaidi ya 26 ni makaa.
Waziri
Makamba alisema hali hiyo inachangia kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo la
mfumo wa kupumua na baadae kusababisha vifo, hivyo ili kukabiliana na hali hiyo
Wizara ya Nishati imetenga shilingi Milioni 500 katika Bajeti yake ya mwaka huu
kwa ajili ya kukabidhiwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuhamasisha matumizi ya nishati
salama.
Alisema REA ndio
taasisi itayosimamia jambo hilo, kwa lengo la kuboresha na kuondoa mzigo katika
sekta ya afya nchini, na kukuza shughuli za kijamii kwa kuongeza fursa za
biashara na ajira, kuwezesha ustawi wa
wanawake na ushiriki wao katika shughuli za maendeleo kikamilifu.
Pia
wamejipanga kuimarisha mifumo ya kisera, kisheria, kiutawala, na kikodi ili kuwezesha watanzania kuondokana
na nishati hiyo inayoathiri afya zao.
Nae Daktari
Bingwa wa Mapafu Dk. Pauline Chale alisema matumizi ya nishati isiyosalama ya
kuni, mkaa na mabaki ya wanyama na mimea yanachangia kuongezeka kwa magonjwa ya
mapafu kutokana kutoa moshi wenye sumu za aina ya kemikali 200 ikiwemo Nitrogen
dioxide gas.
Alisema
moshi huo husababisha magonjwa ya kansa ya koo, mapafu, na kushindwa kupumua
ambapo kusababisha watu karibu bilioni 1.6 duiniani wanapoteza maisha kutokana
na matumizi ya nishati ya kupikia isiyosalama.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Said alisema atahakikisha maeneo yote ya
vijijini yanapata nishati salama ya kupikia, ambapo ndio lengo la serikali katika
kupata vipimo vya maendeleo ya nchi na kwa mwaka huu kutakuwa na uhamasishaji
wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment