Habari za Punde

Mhe Othman akutana na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stergomena Tax


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akimkaribisha waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stergomena Tax alipowasili ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar kujitambulisha kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kitengo cha habari.).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , (kulia) akizungumza na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stergomena Tax alipofika  ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar kujitambulisha kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kitengo cha habari.).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , (kulia) akizungumza na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stergomena Tax alipofika  ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar kujitambulisha kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni.  Kulia kwa waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Maryam Haji Mrisho .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kitengo cha habari.).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stergomena Tax alipofika  ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar kujitambulisha kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni. 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kitengo cha habari.).

 MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika Mashariki kuongeza uelewa kwa wataanzania kuwezesha kuyafahamu masuala mbali mbali muhimu yanayoendelea katika jumuiya za Kimataifa na Kikanda.

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stergomena Tax alieyefika Ofisini kwa Makamu kujitambulisha baada ya uteuzi uliofanywa hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Makamu amesema kwamba yapo masuala mengi na muhimu yanayoendelea katika Jumuiya hizo ambayo watanzania wa kawaida pamoja na viongozi wanapaswa kuyafahamu katika hatua za michakato hadi utekelezaji wake kwa mafunufaa ya watanzania wote.

Mhe. Othman amefahamisha kwamba kufanya hivyo pia ni muhimu kwani kutasaidia  wananchi na Viongozi nchini kuzifahamu fursa mbali mbali za kiuchumi na kimaendeleo zilizopo katika ngazi ya kikanda na kimataifa ili waweze kuzitumia kwa faida yao na taifa kwa jumla.

Mhe. Othman ametolea mfano wa Jumuiya ya Kimataifa  inayoshughulikia Haki Miliki za Wabunifu Duniani (WIPO), kwamba zipo fursa nyingi ambazo kutokana na kukosekana uwelewa kwa wananchi fursa hizo hazitumiki ipasavyo na pia kukosekana uwakilishi wa kuchangia masuala mbali mbali pale inapohitajika.

Akizungumzia suala la Balozi mbali mbali zilizoko katika Kituo cha Kenya ambazo uwakilishi wao pia unafikia Tanzania, kuhakikisha kwamba shughuli na huduma zao wanazotoa zikiwemo za watalii wainafikia Zanzibar ili nchi kuweza kunufaikia kupitia kuwepo kwao Tanzania.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Stergomena Tax, amesema kwamba wizara hiyo itayafanyia kazi maelekezo aliyopewa na kwamba suala la ushirikishwaji wa wananchi katika kujenga uwelewa litawekewa mpango maalumu katika utekelezaji wake.

Amefahamisha kwamba hatua hiyo ni muhimu katika kurahisisha utekelezaji wa masuala mbali mbali yanayotokana na Jumuia za Kikatanda na Kimataifa ambayo nchi imeridhia itifaki zake na pia kusainiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekelezwa nchini.

Akizungumzia suala la mikutano ya mabalozi inayofanyika Tanzania , Waziri Tax amesema kwamba wizara hiyo itahaikisha kuwepo kwa uwiano sawa kwa pande mbili za muungano katika masuala mbali mbali yanayotekelezwa kupitia itifaki za kibalozi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.