Habari za Punde

Bodaboda wanaovunja sheria kukiona Zanzibar

 

NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR                                                             21/11/2022

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema Jeshi la Polisi litawashughulikia kwa mujibu wa sharia madereva wa bodaboda wanaokiuka sharia na taratibu zilisowekwa ikiwa ni pamoja na kutojisajili kwenye vyama na Jumuiya za waendesha bodaboda.

CP Hamad ametoa kauli hiyo huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja alipokua akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Paje, Bwejuu na Michamvi katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi zinazojitokeza katika maeneo yao.

Amesema kutofuata sharia na kutojisajili kwa waendesha bodaboda wengi kunachangia kujihusisha na vitendo vya uhalifu waendesha bodaboda hao na kwamba inakuwa vigumu kudhibitiwa na  Jeshi la Polisi kutokana na kukosekana kwa taarifa zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi wa Polisi Richard Tadei Mchomvu ameitaka jamii kubadili fikra ya kupambana na uhalifu badala yake kuchukua hatua za kuzuia uhalifu katika maeneo yao.

Kwa upande wao wananchi wa Maeneo hayo wamelalamikia videndo vya uvunjwaji wa Sheria vinavyofanywa na waendesha bodaboda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.