Habari za Punde

Manispa ya Iringa Yashika Nafasi ya Pili Usafi wa Mazingira Kitaifa

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada( katikati)akiwa na  Mhe diwani kata ya Mkimbizi kushoto Mhe.Eliud Mvela ,kulia ni diwani viti maalum mhe Hellen Machibya wakifurahia cheti cha mshindi wa Pili wakati wa kilele cha Wiki ya Usafi wa Mazingira Kitaifa na Siku ya Matumizi wa Choo Duniani iliyoenda sambamba na utoaji wa tuzo za Usafi.

Na Fredy Mgunda, Iringa.                                                                                                         
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imeendelea kuboresha majinjio ya kisasa pamoja na kuhakikisha 'madampo'  makuu yanakuwa masafi lengo likiwa ni kuendelea kushika nafasi ya juu au ya kwanza  ya usafi huo  ambapo kwa msimu huu imeshika nafasi ya pili tena katika mashindano ya Usafi wa Mazingira.

Akizungumza jijini Dodoma Novemba 19,2022, mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya ushindi wa usafi wa mazingira, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya  Manispaa  ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada wakati wa kilele cha Wiki ya Usafi wa Mazingira Kitaifa na Siku ya Matumizi wa Choo Duniani iliyoenda sambamba na utoaji wa tuzo za Usafi  huo amesema  awali hawakuwa amachinjio mazuri na ya kisasa  lakini kwasasa tayari wanayo.

Meya huyo ameeleza kuwa jambo jingine lilolowasabishwa wao kushika nafasi hiyo ni jitihada zao za kuhakikisha wanaweka michoro na maandishi ya onyo kila panapostahili.

"Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa tumeendelea kuongoza  kwenye mashindano usafi wa mazingira katika halmashauri zote za Manispaa, msimu uliopita tulikuwa wa pili kitaifa na msimu huu  mwaka 2021/202 tumefanikiwa pia kuwa washindi wa pili," amesema Ngwada. 

Aidha amesema kuwa wanaendelea kuishukuru serikali  kwa kuwatambua wao kama halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kushika  nafasi y a pili kitaifa kw usafi wa mazingira.

Amesema  wanaendelea kuuweka Mji wao wa Iringa safi na kwamba wananchi wa meendelea kuwa na mapenzi na usafi pamoja  na kufanyaji wa usafi wa mazingira katika maeneo yao.

"Leo tumekuja hapa kwa ajili ya kupokea zawadi ya usafi wa mazingira, tunashukuru kupata zawadi, kwanza kutambulika na serikali kuwa Mji wetu wa Iringa ni miongoni mwa Miji misafi,"ameeleza Meya huyo.

Ngwada ameeleza kuwa watahakikisha wanaongeza jitihada za kuendelea kushika nafasi hiyo au kwenda juu zaidi na kwamba wamewndelea kuwashirikisha wananchi wa Iringa kwani usafi ni sehemu ya maisha yao.

Ameongeza kuwa utamaduni wa kufanya usafi si tu siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni kila siku, wanairinga wanafanya usafi wa mazingira na kwamba wamekuwa na makongamano mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa wakazi wa Iringa lengo likiwa ni kuona kuna umuhimu na thamani ya kuendelea kufanya usafi huo katika maeneo yanayozunguka wanapo ishi.

Pia amesema wamekuwa wakizihamasisha shule zao hadi Vyuo vikuu kuendelea kufanya usafi wa mazingira hivyo usafi kwa wanairinga ni utamaduni wao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.