Habari za Punde

Mhe Hemed mgeni rasmi katika Mahafali ya Ishirini na Moja (21) ya Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza na Wahitimu wa Mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na Jumuiya ya Wahitimu waliomaliza Mzumbe katika Mkutano Mkuu wa jumuiya hiyo iliofanyika Kampasi Kuu ya Chuo hicho uliyofanyika ukumbi wa Maekeni.
Naibu Katibu MKuu CCM Bara Christiana Mndema akiwasilisha Mada ya Umuhimu wa  kuwa wamoja wahitimu wa Chuo cha Mzumbe katika Mkutano Mkuu wa Chuo hicho uliofanyika Kampasi Kuu ya Chuo hicho iliyofanyika Ukumbi wa Maekeni Mkoa wa Morogoro
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Saida Yahya Ohman akitoa Salamu zake katika Mkutano Mkuu wa jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe uliofanyika Kampasi Kuu ya Chuo hicho katika Ukumbi wa Maekani Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya Wahitimu na Wanachama wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza kwa makini Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Marekani kampasi Kuu ya Chuo hicho Mkoa wa Morogoro

Na Abdulrahim Khamis OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed sueiman Abdulla amewapongeza Wahitimu wa Mahafali ya Ishirini na Moja (21)  ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa kukamilisha muda wa Masomo Chuoni hapo.

Mhe. Hemed  ameeleza hayo katika Mkutano Mkuu wa Ishirini na Mbili (22) wa Baraza la Masajili la Chuo Kikuu Mzumbe uliofanyika katika Ukumbi wa Maekani   uliopo Kampasi Kuu ya Chuo hicho Mkoa wa Morogoro. 

Amesema ni hatua ya kupongezwa kwa Wahitimu hao kwa kujielekeza kikamilifu katika kujiongezea maarifa na uweledi, jitihada walizoonesha na Wahadhiri wa Chuo hicho zimewasaidia kufikia hatua ya kuhitimu na kuwataka kutumia elimu zao kwa maendeleo ya watu.

‘’Ninawahimiza kuwa Sehemu ya kukitumikia na kukiendeleza  Chuo Kikuu cha Mzumbe, kwa maana ya kwamba muwe Alumni wazuri katika kukitangaza Chuo hichi ’’ amesema

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameupongeza Uongozi wa Chuo hicho pamoja na Uongozi wa Baraza la Masajili kwa jithada mbali mbali wanazochukua ikiwemo kuandaa Katiba ya Wahitimu  (Alumni) Mpango Mkakati wa Alumni kwa lengo la kuendeleza Chuo hicho.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameeleza kuwa hatua ya kuandaa miongozo hiyo zitasaidia kutoa nafasi kwa Wahitimu kukutana na kujadiliana mambo mbali mbali ikiwemo kubadilishana mawazo na uzoefu.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa ni mmoja kati ya waliosoma Chuo Kikuu cha Mzumbe amewataka Wahadhirii wa Chuo hicho kuongeza Juhudi hasa katika kuongeza Machapisho na Tafiti mbali mbali hatua ambayo Taifa litatumia Tafiti na Machapisho hayo katika  kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, kijamii na Kiteknolojia.

Pamoja na hayo Mhe. Hemed ameushauri kuanzishwa kwa Mfuko wa Ufadhili wa Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe utakaowasaidia Watanzania  ambao wana uwezo wa kusoma katika Ngazi ya Chuo Kikuu ambao hushindwa kuendelea na Masomo kutokana na ukosefu wa Fedha.

Mhe. Hemed ameushauri Uongozi wa Chuo hicho kuangalia namna ya kuanzisha Mashirikiano na Vyuo vya Zanzibar ili kutanua wigo wa kuchagua Program za kjiufunza na kusogeza fursa ya Elimu kwa Wazanzibari.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameutaka Uongozi wa Chuo hicho kuwa Sehemu ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kutimiza Malengo ya kujenga na kuiendeleza Tanzania.

Ametua fursa hiyo kuupongeza  Uongozi wa Chuo hicho kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ikiwemo kuzalisha Idadi kubwa ya Wanafunzi wanaofaulu kwa Umahiri Mkubwa na hatimae kupata wasomi wanaoendeleza Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha ameeleza kuwa Mkutano huo hufanyika kila Mwaka kwa lengo la kuwakutanisha kwa kujadili namna ya kuboresha kukuza Chuo pamoja na kuwapongeza Wanafunzi na wWfanyakazi waliofanya vizuri.

Aidha ameeleza kuwa Chuo kimeshaanza kujenga Majengo makubwa eneo la Maekani ikiwemo Jengo la Uongozi, eneo la Michezo pamoja na Ukumbi wa Mahafali.

Akielezea umuhimu wa umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Mzumbe Christina Mndema Ameeleza kuwa kujitolea kwa wahitimu wa chuo hicho kutasaidia kutumia eleimu walioipata kutoa fadhila kwa kukisaidia chuo hicho.

Aidha ameleza kuwa umoja huo pia unasaidia kuwahimiza na kuwajenga wanajumuika hiyo kuwa na uzalendo kwa mustakbali mzuri kwa Taifa.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.