Habari za Punde

Tatizo la afya ya akili huchangia katika ubakaji wa watoto

 Na Maulid Yussuf WMJJWW 


Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto bwana Hassan Ibrahim ameitaka kamati iliyowasilisha ripoti  inayohusiana na masuala ya udhalilishaii kusimamia vizuri majukumu yao ya kazi ili kuondoa tatizo hilo. 

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa  kuwasilishwa ripoti ya miaka mitano ya mwaka 2017hadi 2022, katika Ukumbi wa ZURA Maisara Mjini Unguja.

Amesema watu wenye ulemavu ni vyema wazingatiwe kwenye ripoti hiyo kwani masuala ya udhalilishaji yanapowakuta wanakuwa ni waathirika sana.

Amesema ipo haja kwa watu  wenye ulemavu nao waweze kupatiwa elimu ya masuala ya udhalilishaji ili iweze kuwaongezea uwelewa  pale tatizo nalipowafika na kujua mbinu za kujinginga.

"Tunapaswa kukemea vitendo viovu na kuwatetea wale walofanyiwa vitendo hivyo ili kutokomeza vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto" amesisitiza Mkurugenzi Hassan.

Aidha amefahamisha kuwa kuna tatizo la afya ya akili katika jamii inayotokana na msongo wa mawazo hali inayopelekea baadhi yao kubaka, hivyo ameshauri kuanzishwa kwa vituo vya ushauri nasaha ili waweze kuwasaidia watu wa aina hiyo.

Wakitoa michango yao baadhi ya washiriki wa Mktano huo wamesema,  ripoti hiyo itawasaidia katika utekelezaji kwa kupitia utendaji wao ili kuwapa muelekeo wa mpango kazi  kwa kuweza kupambana juu ya vitendo vya udhalilishaji.

Pia wameomba kufuatiliwa kwa kina baadhi ya polisi waliokuwepo vituoni kwani baadhi yao wamekuwa wakichangia kuendelea kuwepo kwa matukio ya udhalilishaji kutokana na kuwatolea maneno yasiyofaa akina mama wanaofika kuripoti juu ya kudai haki zao za matunzo ya watoto wao.

Hata hivyo wamesema tatizo la talaka limeonekana kuwa ni kubwa hali inayopelekea watoto na wanawake kudhalilika katika kupata mahitaji yao .

Nae Afisa programu za kijinsia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu UNFPA, ndugu  Ali Hammad amesema mpango  kazi wao utaweza kuwasaidia ili kuzuiya udhalilishaji kwa watoto na wanawake na jamii kwa ujumla.

Mpango kazi huo wa 2017-2022, umewasiIishwa kwa lengo la kupata maoni ya wadau kutoka Taasisi za Serikali na za Binafsi ili kuweza kuandaa mpango kazi mpya utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.