Habari za Punde

Viongozi wa Dawati la Jinsia la Chuo cha Al. Sumait Zanzibar Wametakiwa Kutunza Siri za Malalamiko ya Udhalilishaji Watakayoripotiwa na Wananfunzi

Na Maulid Yussuf WMJJWW 

VIONGOZI wa Dawati la Jinsia la Chuo cha Abrahman Al. Sumait wametakiwa kutunza siri za malalamiko ya udhalilishaji watakayoripotiwa na Wananfunzi ili kutoa uwaminifu kwa wanaowasimamia.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi  Siti Abass  Ali wakati alipozindua dawati la jinsia kwa chuo hicho.

Ameema masuala ya udhalilishaji yanahitaji usiri wa hali ya juu, katika utekelezaji wake hasa pale unapoletewa tarifa, hivyo ni vyema kuwaweka watu madhubuti wanaojua masuala mazima ya udhalilishaji.

Hata hivyo amesema kwamba haitakuwa vyema kuona Mwananfunzi amepeleka kesi yake kwa dawati lakini anatoka nje anasikia tayari linazungumzwa hapo uwaminifu hautakuwepo na kila mmoja ataogopa kutoa taarifa.

“Kabla ya kuanza kazi rasmi ni vyema mukajijengea uwaminifu kwa munaowasimamia kwani bila ya kufanya hivyo hamtakuwa na kazi yoyote ya kufanya”, alisema.

Amesema kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vyuo vikuu ni kuhakikisha kwamba kesi zote ambazo zinatokea za udhalilishaji zinaripotiwa hapo.

Mapema wakili wa Kujitegemea kutoka Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) bi Time Asaa Khamis amesema suala la udhalilishaji bado limeenea katika kila pahala ikiwemo katika Vyuo vikuu na ndio maana Serikali imechukuwa juhudi mbali mbali za kuhakikisha linamalizika kwa kuanzisha madawati vyuoni. 

Ameema wazo la kuanzishwa madawati katika vyuo vikuu lilitokana na Jumuiya yao baada ya kuona changamoto za udhalilishaji wanaofanyiwa Wanafunzi wa vyuo hasa wanawake, kupitia sheria namba 13 ya mwaka 2018 ambayo awali iliruhusu kutekelezwa katika vyuo vinavyosomesha sheria na baadae wakaamua sheria hiyo itumike katika Vyuo vyote.
 
Akisoma risala yao  wananfunzi kwa niaba ya kamati ya dawati hilo Mwanafunzi Nuru Salim Fasih, amezishukuru Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuweka mfumo wa dawati la jinsia katika vyuo ili kupambana na matukio ya udhalilishaji. 

Amesema mfumo huo pamoja na kua utawasaidia Wananfunzi wakiwa vyuoni bali watakuwa na uwelewa wa kutoa elimu juu ya vitendo hivyo kwa jamii hata pale watakapomaliza masomo yao.

Hata hivyo ameiomba Serikali kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara na kila panapohitajika ili kuona wanakuwa na uwelewa mpana juu ya vitendo hivyo na kuwa na uweledi wa kulisimamia dawati hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.