Habari za Punde

Wajasiriamali watakiwa kuendelea kuongeza ubunifu na ubora wa bidhaa

Waziri anayesimamia Masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Magode wa Uganda akihutubia kwenye sherehe za kufunga Maonesho ya 22 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Wajasiriamali Wadogo na Wakati, maarufu Juakali yaliyofanyika katika viwanja vya Uhuru vya Kololo jijini Kampala, Uganda.
 Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia musuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akikabidhi cheti kwa mshiriki wa maonesho kutoka Jamhuri ya Congo kwa kufanya vizuri katika ngazi ya kitaifa
 Waziri anayesimamia Masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Magode wa Uganda akibadhiwa shati alilolinunua na mjasiriamali wa Watanzania. 
  Waziri anayesimamia Masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Magode wa Uganda akiangalia bidhaa za mjariamali wa Tanzania kwenye sherehe ya kufunga Maonesho ya 22 ya Juakali iliyofanyika katika viwanja vya Uhuru vya Kololo jijini Kampala, Uganda

Picha ya pamoja na Meza Kuu na Wajasiriamali waliopata vyeti na tuzo za kufanya vizuri zaidi kwenye Maonesho ya 22 ya Juakali yaliyofanyika katika viwanja vya Uhuru vya Kololo jijini Kampala, Uganda

Wajasiriamali wa Wadogo na wa kati wamehimizwa kuendelea kuongeza ubunifu na ubora wa huduma na bidhaa wanazozalisha ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya ushindani katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (African Continental Free Trade Area - AfCFTA). 

 

Haya yamejili leo tarehe 18/12/2022 kwenye sherehe ya kufunga Maonesho ya 22 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Wajasiriamali Wadogo na Wakati, maarufu Juakali yaliyofanyika katika viwanja vya Uhuru vya Kololo jijini Kampala, Uganda. 

 

Akizungumza kwenye hafla ya kufunga maonesho hayo Waziri anayesimamia Masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Magode wa Uganda ameeleza kuwa pamoja na kazi nzuri inayoendelea kufanywa na wajasiriamali, wasiridhike na hatua ya mafanikio waliyoifikia bali waendelee kuongeza ubunifu na ubora zaidi wa huduma na bidhaa wanazozalisha ili kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindani hasa katika nyakati hizi za soko huria. 

 

Waziri Magode aliendelea kueleza kuwa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya wanaendelea kutengeneza mazingira wezeshi zaidi kwa wafanyabiashara ili waweze kuendesha shughuli zao kwa uhuru na kwa faida zaidi.

 

Katika ngazi ya Jumuiya Nchi Wanachama kwa kushirikiana na Sekretarieti na wadau wengine sote tumekubaliana na tunaahidi kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uendeshaji ya biashara yatakayowezesha  Wafanyabishara wadogo, kati, wa kubwa sio tu kunufaika na soko la Afrika Mashariki bali soko kubwa la Afrika katika mpango wa AfCFTA”

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia musuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote ametoa rai kwa Jumuiya kuendelea kuenzi na kutumia lugha ya Kiswahili katika kuendesha biashara kwa kuwa ndiyo lugha pekee itayako wezesha kuunganisha wafanyabiasha wengi zaidi katika Jumuiya na kurahisisha ufanyaji wa biashara.  

 

Vilevile Mahandisi Mlote ameeleza kuwa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imepokea mapendekezo ya wajasiriamali, ya kuomba maonesho hayo yafanyike walo mara mbili kwa mwaka kutokana na umuhimu wake. Alieleza kuwa mapendekezo hayo yamepokewa na yataafikishwa katika ngazi husika kwa mashauriano na maamuzi zaidi.

 

Sherehe za kufunga maonesho hayo ziliambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo ugawaji wa zawadi kwa washiriki waliofanya vizuri zaidi, vyeti vya ushiriki na burudani mbalimbali. 

 

Aidha, Jamhuri ya Burundi imepewa dhamana ya kuandaa maonesho yajayo ya 23 ya Afrika Mashariki ya Wajasiriamali Wadogo na Wakati yanayotarajiwa kufanyika mwakani 2023. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.