Habari za Punde

Wakili Mpanju Aawapa Majukumu Jukwaa la Kitaifa la Malezi Mbadala

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amin Mpanju akifungua kikao cha Siku tatu cha Jukwaa la Malezi Mbadala lilikutana mjini Morogoro kwa ajili yakuweka Mikakati ya Malezi Mbadalakuanzia
Washiriki wa kikao cha Wadau wa Jukwaa Mbadala la Malezi wakiwa wanafatilia na kusiliza kwa Umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi Wakili Amin Mpanju Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati wa hotuba yake.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amin Mpanju akiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kikao cha Siku tatu cha Jukwaa la Malezi Mbadala lilikutana mjini Morogoro kwa ajili yakuweka Mikakati ya Malezi Mbadala kuanzia Disemba, 08-10, 2022.
 ( Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini)

Na WMJJWM, Morogoro.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, alimelitaka Jukwaa la Kitaifa la Malezi mbadala kutoka na mbinu itakayosaidia kuwanusuru watoto wanaopitia madhila mbalimbali katika hatua za makuzi na kujikuta wapo eneo la Malezi Mbadala.

Wakili Mpanju ametoa wito huo leo Disemba 09, 2022 wakati akifungua kikao kazi kati ya Serikali na wadau mkoani Morogoro.

Mpanju amemtaka Kamishana wa Ustawi wa Jamii, kuhakikisha Jukwaa hilo linakuwa na Uongozi utakaowezesha kuwakutanisha mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kuona ni mikakati ipi itakayosadia kwenye suala la Malezi Mbadala.

“Kamishna hakikisha Jukwaa hili linasimamiwa ipasavyo, hakikisheni, linakutana Mara mbili kwa Mwaka, tengenezeni Muundo, wekeni Mikakati na Mbinu zipi zitumike kuboresha Malezi ya Mtoto, aidha mhakikishe Jukwaa likafika hadi ngazi ya Vijiji na Mitaa” amesema Mapanju.

Katika hatua nyingine Wakili Mpanju ametaka suala la Malezi Mbadala liwe ni suala la mpito, kwani anaamini kuwa kila Mtoto aliye ndani ya Jamii ana mlezi wake hivyo Jamii isichululie suala la Malezi Mbadala kama ndio suluhisho la kudumu.

“Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2019, kifungu cha 16 na 144. Watoto wanaohitaji huduma ya Malezi mbadala ni Watoto wanaoishi katika Makao ya Watoto na Watoto waliokinzana na Sheria, Watoto wanaoambatana na mama zao Gerezani, Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani au wanaombata na mzazi/mlezi ambaye anaomba mitaani, Watoto wanaoishi katika familia ambazo mkuu wa kaya ni mtoto, Mtoto anayeishi na mtu ambaye ni mgonjwa, mlemavu au mzee ambaye anashindwa kukidhi mahitaji ya msingi, Watoto walio katika hatari ya kufanyiwa ukatili wakiwepo wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu” amesema Mpanju.

Wakili Mpanju ameongeza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbali mbali katika utoaji wa huduma ya malezi mbadala.

“Hadi sasa jumla ya Mkao ya watoto 325 yamesajiliwa yakiwemo mawili  ya Serikali yenye Jumla ya watoto 9011 Wavulana 4897 na Waschana 4114, aidha serikali imeendelea kuratibu huduma ya malezi ya Kambo na Kuasili ambapo kwa kipindi cha 2020/21 Wizara ilipokea maombi 110  jumla ya watoto 40 waliwekwa kwenye Malezi ya kambo na watoto 50 waliasiliwa wakiume 28 na wakike 22 ikilinganishwa na maombi 131 ambapo jumla ya watoto 48 wakiume21 wakike 27 waliwekwa kwenye malezi ya kambo na watoto 56 waliasiliwa wakiume 17 wakike 39 kwa mwaka 2021/22.

Wakili Mpanju, ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI, kutumia mifumo Madhubuti ya TEHAMA, itakayosaidia kuweka takwimu sahihi kwa kuwabaini watoto wanaohitaji Malezi mbadala.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mariam Nkumbwa, amesema watahakikisha wanaimarisha mifumo ya Ufuatiliaji na shughuli zote za Malezi zinaingia kwenye Mipango ya bajeti sambamba na kuimarisha ushirika na wadau ili kuwa na takwimu sahihi.

Naye mwakilishi wa Shirika la SOS Onesmo Itozya amesema,Usalama wa Watoto wa leo ndio Usalama wa Taifa la kesho, wao kama SOS ambao wamekuwa nchini  kwa zaidi ya Miaka 30 bado wanaiona ipo haja suala la Malezi Mbadala likapewa kipaumbele.

“Toka kupata kwa Uhuru wa Nchi yetu, leo tukiwa tunatimiza Miaka 61, nafurahi kwa mara ya kwanza tunakuwa na jukwaa la pamoja la kujadili masuala ya Malezi Mbadala hii haijawahi kutokea, hivyo tutatumia fursa hii tuweze kutoka na afua zitakazo weza kulinusuru taifa na watu waliokosa Malezi bora” amesema Itozya.

Awali akitoa Salaama za Mkoa, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Wahida Ntiro amesema anaipongeza Serikali kwa hatua hiyo huku akiomba Wizara kuongeza Wataalam wa Ustawi wa Jamii kwenye ngazi za Mikoa na Halmashauri ili kuwezesha shughuli hizo kutokukwama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.