Habari za Punde

Michuano ya 17 ya Kombe la Mapinduzi Kati ya Singida Big Star na KMKM Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Singida Imeshinda Bao 2--0

Kipa wa Timu ya KMKM akiwa na mpira wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Unguja.Timu ya Singida Big Star imeshinda mchezo huo kwa bao 2--0, uliofanyika jana usiku katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja.

Katika chezo huo Timu ya Singida Big Star imefanikiwa kuandika bao lake la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Bruno Gomes katika dakika ya 20 ya mchezo huo kipindi cha kwanza 
Singida Big Star wamefanikiwa kuandika bao la pili na la ushindi kupitia mchezaji wake Yussuf Kagoma katika dakika ya 34 ya mchezo huo kipindi cha kwanza. 
Wachezaji wa Timu ya KMKM wakiwa katika Uwanja wa Amaan wakisubiri kusalimiana na mgeni rasmin wa mchezo huo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Bi.Hamida Mussa Khamis.katika mchezo huo Timu ya Singida Big Star imeibuka mshindi kwa bao 2--0.
Kikosi cha Timu ya Singida Big Star wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi na Timu ya KMKM uliofanyika jana usiku na kuibuka na ushindi wa bao 2-0
Kikosi cha Timu ya KMKM wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi na Timu ya Singida Big Star uliofanyika jana usiku katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja na kukubali kipigo cha bao bao 2-0 katika mchezo huo wa Mapinduzi Cup.
Waamuzi wa Mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Singida Big Star na KMKM wakiwa katika picha ya pamoja na Captan wa timu hizo kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika jana usiku katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Jijini Zanzibar.

Wachezaji wa Timu ya Big Star wakipasha kabla ya kuaza kwa mchezo wao kuwania Kombe la Mapinduzi na Timu ya KMKM uliofanyika jana usiku Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.