RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bwa.Emmanuel Tutuba, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Uongozi wa BOT kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 18-1-2023, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu na (kulia) Gavana Mstaafu wa BOT Prof. Florens Luoga.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania ukiongozwa na Gavana wa BOT Bwa.Emmanuel Tutuba, (kulia kwa Rais) na (lushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Emmanuel Tutuba (kulia kwa Rais) akiwa na Gavana Mstaafu wa (BOT) Prof Florens Luoga , alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 18-1-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw.Emmanuel Tutuba na Gavana Mstaafu wa (BOT) Prof. Florens Luoga, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 18-1-2023.(Picha na Ikulu)
NA MWASHAMBA
JUMA, IKULU
MSARIFU
wa taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation (BMF), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameueleza uongozi wa taasisi
hiyo, kuendelea kuboresha mifumo ya afya kwenye taasisi yao ili kutoa huduma
bora kwa wananchi.
Aidha, aliutaka uongozi huo kuangalia kwa upana jinsi ya
kukamilisha miundombinu ya vifaa tiba pamoja na kuimarisha mifumo ya
mawasiliano itakayotoa huduma bora kwa walengwa na kuboresha utendaji kwa
kuongeza nguvukazi za ajira ili kutanua wigo kwenye taasisi hiyo.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipokutana na uongozi na
wafanyakazi wa taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation Ikulu, Zanzibar.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza
ushirikiano wake na taasisi hiyo katika kuimarisha huduma bora za afya pamoja
na kupongeza juhudi za BMF katika utendajikazi wake nchi nzima, Bara na
Zanzibar.
Mbali na kusifu jitihada zinazochukuliwa na uongozi kwa kuisimamia
vyema taasisi hiyo, pia Dk. Mwinyi aliwataka watendaji na wafanyakazi wa BMF
kuanzisha bima ya afya kwa lengo la kwenda sambamba na mahitaji ya wananchi.
“Wenzetu kule Bara
washaanza kutoa bima ya Afya na sisi Zanzibar tunakaribia kuanza” Rais Mwinyi
aliuelezea uongozi wa BMF.
Katika hatua nyengine Rais Dk. Mwinyi aliwatunuku vyeti,
tunzo na fedha taslimu wafanyakazi
waliofanya vizuri kwenye taasisi hiyo kwa kipindi cha utumishi wao pamoja na
kuwapongeza.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini ya BMF, Balozi Tuvako Manongi alisema, bodi yao imeendelea
kushirikiana kwa karibu na taasisi mbalimbali zikiwemo Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wadau wa maendeleo wakiwemo
wafadhili kutoka sekta za umma na binafsi pamoja na wachangiaji binafsi katika kuhakikisha
wanapata rasilimali fedha.
Naye, Ofisa Mtendaji mkuu wa BMF, Dk. Ellen Senkoro
alisema taasisi imekusudia kuvitekeleza vipaumbele vyake vinne ikiwemo
kuufanyia tathmini ya Mpango Mkakati uliopo wa taasisi hiyo ili kuongeza
ubunifu na wigo wa kuanzisha miradi mipya baada ya mikongwe iliopo kukamilika
kwa asilimia 50.
Aidha, alieleza wanaboresha utendaji wa taasisi hiyo kwa
kutumia teknolojia za kisasa ili kupunguza gharama za uendeshaji na kufanyakazi
kwa weledi na kuongeza kuwa walifanikiwa kutekeleza miradi mikubwa na midogo
kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 ambayo iliboresha huduma za afya kwa mikoa 25
ya Bara na mitano ya Zanzibar, ikiwemo kuongeza rasilimali watu, kuimarisha
miundombinu ya majengo na vifaa tiba pamoja na kukabiliana dhidi ya mapambano
ya Ukimwi, kifua kikuu na UVIKO 19.
Hata, hivyo aliahidhi kuendeleza ushirikiano uliopo baina
ya taasisi hiyo na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kufanikisha dira ya
taasisi yao.
Taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation iliasisiswa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa ambayo imebeba maono na sifa za viongozi bora wa Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment