Habari za Punde

Watu 104 Wamefariki Dunia kwa Ajali za Barabarani

Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa Mjini Magharibi Unguja ASP. Hamis Mwakanolo akizungumza kuhusu ajali za barabarani  na Ujumbe kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  huko ofisini kwake Madema

Na Khadija Khamis -Maelezo  Zanzibar.

Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa Mjini Magharibi Unguja ASP. Hamis Mwakanolo amesema watu 104 wamefariki dunia katika ajali za barabarani zilizoripotiwa katika mkoa huo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita  .

Kamanda Mwakanolo alieleza hayo wakati alipokuwa na mazungumzo   na Ujumbe kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa huko ofisini kwake Madema.

Amesema jumla ya matukio ya ajali 112 yameripotiwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2022 ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi .

Hata hivyo alisema licha ya kuongezeka kwa ajali za barabarani lakini idadi ya vifo  imepungua,ambapo katika kipindi hicho jumla ya makosa 18909 yameripotiwa .

Kamanda huyo aliyataja maeneo ambayo yamekuwa yakitokea ajali za mara kwa mara ni pamoja na barabara ya Fumba ,Mwera,Mfenesini na barabara ya Mkapa Darajabovu .

Aidha aliueleza ujumbe huo kuwa Jeshi la Polisi la Mkoa wa Mjini Magharibi linaendelea kutoa elimu juu ya matumizi salama ya barabarani kwa lengo la kupunguza kiwango cha ajali za barabarani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.