Na.Rashid Omar.OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewagiza viongozi wa Manispaa ya Mjini
Unguja kuifanyia kazi mara moja changamoto ya uchafu uliopo katika maeneo mbali
mbali ya biashara katika maeneo ya mjini hapa.
Mhe. Othman ametoa agizo hilo alipotembelea
biahara mbali mbali zinazoendelea wakati huu waislam wakiwa katika maandalizi
ya siku Kuu ya Eid El-fitry wakati Wumini wa dini hiyo Duniani kote wakielekea kukamilisha Funga ya
mwenzi mtukufu wa Ramadhani .
Mhe. Othman alitembelea maduka ya
biashara mbali mbali za mahitaji ya wananchi kwa ajili ya sikuu Kuu hiyo ikiwemo
, nguo za watoto , viatu, mpazia, kazu za kiume na nyengine kadhaa kuona hali halisi ya bidhaa hizo , bei
na upatikanaji wake sambamba na kuelewa
changamoto za kibiashara zilizopo katika mitaa maarufu ya Mlandege, Mchangani,
Mbuyuni na Darajani Zanzibar.
Aidha Mhe . Othman amesema kwamba
katika maeneo mbali mbali aliyotembelea
kumekuwa na hali ya uchafu kwa kuwepo taka zilizochanganyika na maji ya mvua jambo ambalo linapaswa
kushughulikiwa haraka ili kuhakikisha mazingira salama ya biashara na shughuli
nyengine za wananchi mjini hapa.
Mhe. Makamu amefahamisha kwamba
katika kipindi hiki cha maandalizi ya Siku kuu kumekuwa na idadi kubwa ya watu
waofika madukani na hivyo kuwepo msongamano mkubwa wa wananchi waotafuta
mahitaji yao mbali mbali na kwamba suala la usafi nalo lazima lipewe kipaumbele
na wahusika.
Mhe. Othman amesema kwamba ziara
hiyo pia imesaidia kuzifahamu changamoto mbali mbali za wafanyabisahara ambazo
zinahitaji kufanyiwa kazi katika kujenga ustawi na taswira njema katika kuweka
mazingira bora zaidi ya kibiashara hapa Zanzibar.
Amesema kwamba katika ziara hiyo
wafanyabiashara kadhaa wameibua
changamoto mbali mbali ambazo serikali inawajibu wa kuzifanyia kazi na , kutoa maelekezo kwa baadhi ya changamoto
hizo ili kuwepo na utaratibu na
mazingira bora ya uendeshaji shughuli za kibiashara nchini.
Mapema baadhi ya wafanyabiashara
walileleza kwamba bado kunachangamoto katika suala la ulipaji kodi kutokana na
baadhi ya watumishi wa Mamamlaka ya Kodi kuwa na Mtindo wa kuwavizia jambo
ambalo linajenga taswira mbaya kati ya mlipa kodi na mamalaka husika.
Aidha wapo baadhi ya
wafanyabiashara walioshauri kwamba licha ya kazi kubwa kufanyika lakini kuna
haja kubwa kwa mamlaka za bishara kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi
katika suala zima ulipaji kodi na wananchi kudai , kuewa na kuchukua risiti
baada ya kununua bidhaa
Kwa upande mwengine baadhi ya
wafanbyabaiashara walilalamikia hali ya uchafu taka zinaotupwa holela
uliochanganyika na maji ya mvua uliopo katika maeneo mbali mbali ya biashara
hasa ikizingatiwa kwamba hiki ni kipindi cha mvua jambo ambalo linaweza
kuhatarisha afya za wananchi wanofuata huduma kwenye maeneo hayo.
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake cha Habaeri leo tarehe 20/04.2023.
No comments:
Post a Comment