Habari za Punde

Mawakili Wapata Mafunzo Kuhusu Uwasilishaji wa Hoja Mahkamani

Hakimu wa Serikali Zubeir Ali Awamu akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuhusiana na kada ya sheria  wakati wa muhadhara (mafunzo) wa Sheria uliohusu  Uwasilishaji wa Hoja mbele ya Mahakama(SUBMISSION) huko  ZSSF Kariakoo Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa  wa mhadhara (mafunzo) wa Sheria uliohusu Uwasilishaji wa Hoja mbele ya Mahakama(SUBMISSION) wakifuatilia mhadhara huo uliofanyika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar.

Na Maelezo          

Mawakili na Wanasheria wamehimizwa kujiendeleza  kielimu katika fani zao ili kuwa na taaluma zaidi ya  kuendesha kesi mahakamani.

Hayo yamesemwa na Rais wa Chama cha wanasheria Zanzibar Slim Said Abdallah wakati alipokua akifungua Mhadhara (Mafunzo) wa Sheria kuhusu  Uwasilishaji wa Hoja mbele ya Mahakama(SUBMISSION) katika Ukumbi wa  ZSSF Kariakoo.

Amesema  wakili lazima awe na taaluma  na ujunzi  wa hali ya juu katika  kuendesha kesi mahakamani kwa kutumia kanuni na sheria za mawakili  ili jamii iweze kumuamini na kumkubali katika utekelezaji wa majukumu yake , na kuongeza kuwa  endapo wakili atakosa utaalamu huo hutaweza kufanya kazi zake kwa ufanisi .

Aidha amefahamisha kuwa lengo la muhadhara huo ni kuwajengea uwezo mahakimu,majaji, mawakili na makadhi katika utendaji wao ili kuweza kwasilisha kesi katika mahakama.

Amefafanua kuwa  kazi ya uwakili imegawika katika sehemu mbili ikiwemo kukushanya data  sehemu tofauti (Research) na kuziwasilisha   kwa ufanisi ili ziweze kufahamika.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wahusika katika kada ya sheria kwa kuwawezesha mawakili kufanya vizuri katika kazi zao na kuleta tija kwa wanafunzi wa Skuli hiyo hadi kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nae hakimu wa Serikali Zubeir Ali Awamu amesema kuwa mafunzo hayo yataleta faida kubwa hasa kwa  makadhi kwani wameweza kupata elimu kuhusu uwasilishaji katika mahakama jambo ambalo litaondosha usumbufu katika kazi.

Akizungumzia kuhusu uwajibishwaji Zubeir amefahamisha kuwa mwanamke anaweza kushiriki katika kesi ikiwa kulikua na kikundi cha watu fulani na akashuhudia tukio husika hivyo  ipo haja kwa watoto wa kike  kuwajibishwa ikiwa amefanya kosa .

Amefafanua kuwa mtoto wa kike anaweza  kuwajibishwa ijapokuwa adhabu haitofanana na mwanamme kwani kufanyiwa hivyo  ataweza kujikinga na kujiepusha na vitendo viovu jambo ambalo litasaidia kujilinda kuingia katika vitendo hivyo.

Hata hivyo Zubeir amewataka Mawakili wenzake wa  Serikali na wakujitegemea kuendelea  kujifunza zaidi  ili kukabiliana na kesi ya aina na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Akiwasilisha Mada ya Uwasilishwaji Hoja mbele ya Mahakama Jaji  Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof: John Ruhangisa amesema kuwa wakili mzuri lazima awe na elimu ya kutosha na kufahamika wakati  anapowasilisha kazi zake .

Mafunzo ya hayo yameandaliwa na Skuli ya Sheria Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbalimali wakiwemo Majai, Mahakimu, Mawakili, Makadhi na Wanafunzi wa Skuli hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.