Habari za Punde

Mbio za Mwenge Zaridhia Mradi wa Ujenzi wa Soko Mkwajuni

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa  2023 Abdalla Hashim Kaimu  akizungumza na wananchi wa mkwajuni wakati alipokua akifunga mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni miongoni mwa harakati za mbio za mwenge huko mkwajuni wilaya ya kaskazi "A" mkoa wa kaskazini unguja.

Na Rahma Khamis,Maelezo Zanzibar 

Viongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdalla Shaibu Kaimu amemtaka Mkandarasi wa  mradi wa ujenzi wa Soko la Wajasiriamali Mkwajuni kuhakikisha unakamilika kwa wakati .

Ameyasema hayo wakati alipokua akitembelea  na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko hilo huko Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa kaskazini Unguja.

Amesema kuwa ujenzi mzuri ni ule wenye kuzingatia ubora na viwango vya hali ya juu ili wananchi wapate miradi mizuri  na yenye  kudumu kwa muda mrefu.

Amefahamisha kuwa  lengo la matembezi hayo  ni kuangalia ubora pamoja  na kutambua thamanu ya fedha zilizotumika  katika ujenzi huo kama zinaendana na mradi husika.

Shaibu amefafanua kuwa dhamira ya Serikali ni njema kwani inapambana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwemo za masoko ambayo  yataasaidia vijana kujiwezesha kiuchumi.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa soko  hilo Msimamizi wa soko hilo Hassan Abdulrahmani  Hamdu amesema kuwa soko hilo ni la  Wajasirsiamali wa Mkwajuni  na linatarajiwa kukamilika   Agosti 2023 mwaka.

Msimamizi ameeleza kwamba  katika soko hilo litajumuisha sehemu mbalimbali ikiiwemo  milango ya maduka ,mikahawa, Ofisi ,Ukumbi wa mikutano na kibanda cha mlinzi na kuweza  kuhudumia wananchi 400 hadi 500 katika Wilaya hiyo.

Ameongeza kuwa wameamua kujenga soko hilo baada ya kuona wanapata usumbufu wa kukosa mahitaji muhimu ikiwemo bidhaa za sokoni.

Ujenzi huo umegharimu zaidi ya sh za kitanzania milioni 7 na umejengwa chini ya usimamizi wa Mkandarasi kutoka Chuo cha Mafunzo ambapo ujenzi unaendelea.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa   Abdalla Hashim Kaimu akitembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa  soko  la wajasiriamali unaoendelea kujengwa na chuo cha mafunzo Zanzibar wakati mbio za mwenge zilipopita katika mradi huo uliopo  Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa Kaskazini Unguja



Msimamizi wa majengo sBaraza la mji kaskazini "A" Hassan  Abdurahman Hamdu akitoa taatifa fupi kuhusiana  na ujenzi wa soko la wajasiriamali mkwajuni wakati walipotembelewa na mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa,





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.