MAKAMU wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba athari za
kimazingira zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi bado ni changamoto na tishio kubwa la kimazingira linaloendelea
hapa Zanzibar licha ya serikali kufanya juhudi kadhaa kukikabili hali hiyo.
Mhe. Othman
ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na Ujumbe wa Shirika Aga Khan
Foundation ulioongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika
hilo hilo Riaz Nathu.
Kikao hicho kililenga kufanya mashauriano ya
mashirikiano juu ya masuala mbali mbali yaliyochini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza
wa Rais ikiwemo suala la changamoto ya mazingira, madawa ya kulevya, Ukimwi na
mabadiliko ya Tabia nchi ambayo ni masuala mtambuka yanayosimamiwa na ofisi
hiyo.
Mhe. Othman
amesema kwamba athari zinazotokana na janga la kimazingira linaendelea kuwa
changamoto kubwa duniani hasa katika nchi za Visiwa ikiwemo Zanzibar ambapo maeneo
mbali mbali zikiwemo fukwe hasa katika kanda za utalii Unguja na Pemba
yanaendelea kuharibika kutokana na athari za kimazingira.
Amefahamisha
kwambva hivi sasa katika maeneo kama vile ya Jambiani , Nunguwi na sehemu
nyengine za Pemba kama vile Tovuni Kaskazini Pemba ni miongoni mwa maeneo
ambayo mmongonyoko wa fukwe unaendelea
kuathiri maeneo hayo licha ya jitihada mbali mbali za serikali na washirika wa
maendeleo zinazochukuliwa kukabiliana na hali hiyo kuendelea.
Mhe. Makamu
amesema kwamba hata hivyo , jitihada za
Serikali zimesaidia wakulima zaidi ya 200 wa Bonde la Tovuni Kiungoini Pemba kurejea katika mashamba yao kuaendelea
na shughuli zao za kilimo cha mpungu wa kutegemea mvua
ambapo kabla ya juhudi hizo wakulima hao walishindwa kuendeleza kazi ya
kilimo hicho kutokana na mashamba hayo
kuingiwa na maji ya chumvi.
Amefahamisha
kwamba hatua ya kuwarejesha wakulima hao kuendelea na kilomo cha mpunga katika
bonde hilo la tovuni ni mafanikio makubwa ambapo pia ni matokeo ya
juhudi za serikali na washirika mbali mbali wa maendeleo katika kusaidiana kuzikabili ipasavyo
changamoto na athari za mabnadiliko ya tabia nchini.
Amesema
kwamba kutokana na hali hiyo serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea
kuwakaribiasha na ipo tayari kushirikiana na washirika mbali mbali wa maendeleo
katika kuasaidia juhudi za pamoja za
kukabilia hali hiyo na kuweza kupunguza athari zinazoendelea.
Amefahamisha
kwamba hivi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kutekeleza Mradi
mkubwa wa Kitaifa wa kuirejesha Zanzibar kuwa ya Kijani ambapo juhudi za serikali na washirika wa maendeleo
zinahitajika sana kuunga nguvu katika kufanikisha utekelezaji wa suala hilo.
Ameufahamisha
ujumbe huo kwamba dhamira ya Serikali katika mradi huo ni kuwajenga wanajamii wa Zanzibar kuanzia
watoto maskulini kupanda na kuithamini miti ya aina mbali mbali kuiwezesha Zanzibar kuwa
ya kijani ambapo shughuli hiyo inakusudia kuwa shirikishi kwa wadau mbali mbali
wakiwemo wananchi na mashirika ya aina tofauti kama vile shirika la Aga Khan Foundation.
Kwa upande
wake Mtendaji Mkuu wa Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki Riaz Nathu,
ameipongeza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake inazozishukua
katika kukabiliana na suala hilo pamoja na kuwakaribisha washirika wa maendeleo
kusaidiana na juhudi hizo katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabia
nchini.
Amefahamisha
kwamba kutona na hatua hiyo Shirika la Aga Khan Foundation nalo lipo tayari
kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika maeneo mbali mbali ili kwa pamoja
kupunguza athari zitokanazo na chamgamoto ya Mabadiliko ya tabia nchi.
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
28, Julai
2023.
No comments:
Post a Comment